Yearly Archives: 2021

Ongezeko la rizki

Sahl bin Sa'd (radhiyallahu ‘anhu) ameripoti kwamba kuna wakati mmoja, sahaba mmoja alimfata Nabii wa allah (sallallahu alaihi wasallam) Na akalalamika juu ya umasikini na ugumu wa kupata rizki. Nabi wa Allah (sallallahu alaihi wasallam) akamuambia huyu sahaba, "pindi unapo ingia nyumbani kwako, kuwepo watu ndani au hata kama hamna watu ndani basi toa salaam. Baada ya hapo nitumie mimi salaam na soma Qul-Huwallah (surah ikhlaas) mara moja". Sahaba akafanya jinsi alivyo amrishwa na Nabii wa allah (sallallahu alaihi wasallam), na Allah subhaana wata'alah akambariki kwa utajiri mwingi na akaanza kutumia kwa majirani na ndugu zake.

Soma Zaidi »

Kupokea Cheti cha Uhuru kutokana na Unafiki na moto wa Jahannam

Anas (radhiyallahu anhu) ameripoti kwamba Nabii wa Allah (sallallahu alaih wasallam) amesema, "yoyote atakae nitumia salaam mara moja, kwa kumlipa Allah subhaana wata'alah atamtumia salamu mara kumi (yaani: ataampa zawadi na atamfariji na rehma zake), na yoyote atakae nitumia salaam mara kumi, Allah subhaana wata'alah atamtumia salaam mara mia (yaani: ataampa zawadi na atamfariji na rehma zake), na yoyote atakae nitumia salaam mara mia, Allah subhaana wata'alah Atamwandikia (cheti) uhuru, katikati ya macho yake mawili, kutokana na unafiki, (na cheti ya) uhuru kutokana na moto wa jahannum, na Allah subhaana wata'alah ataampa heshma na faraja ya kuwa na mashahidi siku ya qiyamah."

Soma Zaidi »

Njia Za Sunna Za Kufanya Udhu – Sehemu Ya Nane

24. Usitumie maji vibaya ukiwa unafanya udhu.

Sayyidina Abdullah Bin Amr (radhiyallahu anhu) ameripoti kwamba Nabii wa Allah (sallallahu alaih wasallam) alipita kwa Sayyidina Sa'd (radhiyallahu anhu) akiwa anafanya udhu. Nabii wa Allah (sallallahu alaih wasallam) alimuuliza, "huu uharibifu ni wanini (ya maji kwenye udhu wako)?" Alijibu, "kwani kuna uharibifu kwenye udhu?" Nabii wa Allah (sallallahu alaih wasallam) alimjibu, "ndiyo hata kama unafanya udhu ukingoni mwa mto (pia, kuwa makini kutoharibu maji).

Soma Zaidi »