Sunna na Adabu

Njia Za Sunna Za Kufanya Udhu – Sehemu Ya Nane

24. Usitumie maji vibaya ukiwa unafanya udhu.

Sayyidina Abdullah Bin Amr (radhiyallahu anhu) ameripoti kwamba Nabii wa Allah (sallallahu alaih wasallam) alipita kwa Sayyidina Sa'd (radhiyallahu anhu) akiwa anafanya udhu. Nabii wa Allah (sallallahu alaih wasallam) alimuuliza, "huu uharibifu ni wanini (ya maji kwenye udhu wako)?" Alijibu, "kwani kuna uharibifu kwenye udhu?" Nabii wa Allah (sallallahu alaih wasallam) alimjibu, "ndiyo hata kama unafanya udhu ukingoni mwa mto (pia, kuwa makini kutoharibu maji).

Soma Zaidi »

Njia Za Sanna Za Kufanya Udhu -Sehemu Ya saba

20. Osha viungo vya upande wa kulia kabla viungo vya upande wa kushoto.[1] عن أبي هريرة رضي الله عنه قال قال رسول الله صلى الله عليه وسلم إذا لبستم وإذا توضأتم فابدءوا بأيامنكم (سنن أبي داود، الرقم: ٤١٤١)[2] Sayyiduna Abu Hurairah (radhiyallahu anhu) ameripoti kwamba Sayyiduna Rasulullah (sallallahu alaih wasallam) …

Soma Zaidi »

Sunna Na Adabu Za Ramadhaani 5

27. Kaa kwenye itikafu siku 10 za mwisho za ramadhaani kama unauwezo.

Sayyidina Ibnu Abbaas (radhiyallahu ‘anhu) ameripoti kwamba Nabii wa Allah (sallallahu ‘alaihi wasallam) alisema kuhusu mwenye kukaa itkafu, "mwenye kukaa itkafu (ndani ya msikiti) anajiepusha na madhambi, na kwa wakati wote, anapata thawabu ya kufanya ibada mbali mbali angekuwa na uwezo wa kuzifanya kama asingekuwa kwenye itkafu".

Soma Zaidi »

Sunna Na Adabu Za Ramadhaani 4

21. Kuna baraka nyingi kwa kuamka muda wa daku. Kwa hiyo mtu atimize sunna ya daku kabla kuanza kufunga.

Sayyidina Abuu Sa'eed Khudri (radhiyallahu ‘anhu) ameripoti kwamba Nabii wa Allah (sallallahu ‘alaihi wasallam) amesema daku inabaraka nyingi. Kwahiyo usiache sunna ya daku, hata kama mtu anaweza kunywa tonye moja la maji muda wa daku (inabidi mtu afanye hivyo ili atimize sunna ya daku.) Kwa hakika Allah subhaana wata'alah ananyunyizia rehema zake maalumu juu ya wale ambao wanaamka muda wa daku na malaika wanawaombea dua maalumu).

Soma Zaidi »

Sunna Na Adabu Za Ramadhaani 3

15. Kwenye mwezi wa ramadhaani, jaribu kuzidisha kwa wingi matendo mazuri. Imepokelewa katika hadith kwamba ibada yoyote ile ya nafili (matendo mazuri ya hiyari) yaliyofanyika katika mwezi wa ramadhaani, inamchumia mtu thawabu ya kitendo cha faradhi, na thawabu ya kitendo cha faradhi kilicho fanyika katika mwezi wa ramadhaani kinazidishwa mara sabini

Soma Zaidi »

Sunna Na Adabu Za Ramadhaani 2

8. Kwa ukaribio wa ramadhaani na pia kwenye ramadhaani, inabidi mtu asome dua ifuatayo

ewe Allah! Nilinde kwa ajili ya ramadhaani, (kwa kunifanya niuone mwezi wa ramadhaani nikiwa na afya na nguvu ili niweze kuchukuwa maximum faida ndani yake,) na nilindie mwezi wa ramadhaani (kwa kufanya ndani yake nipate maximum faida) na unikubalie.

Soma Zaidi »