Anas (radhiyallahu ‘anhu) anaripoti kuwa Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) alisema, "kuna kundi la malaika wa Allah subhaana wata'ala ambao wanaendelea kuzunguka kote ulimwenguni, wakitafuta mikusanyiko ya dhikr (mikusanyiko ya kumkumbuka Allah subhaanawata'ala). Wanapopata mkusanyiko kama huo, wanakusanyika karibu nao, na baada ya hapo wanatuma wamalaaika wambele miongoni mwao mbinguni (kuripoti kwa Allah subhaana wata'ala). malaika hawa wanamwambia Allah subhaana wata'ala, "Ewe Mola wetu tulifika kwenye kundi la waja wako ambao wanachukulia neema zako kama neema kubwa juu yao, wanasoma kitaabu chako, wanatuma salaam kwa Nabii wako (sallallahu ‘alaihi wasallam) na wanakuomba kwa mahitaji yao yanayohusiana na aakhera na dunia." Allah subhaana wata'ala Atajibu "wazungushie kwa rehema zangu." Malaika kisha huwasilisha, "ewe Mola! kati yao kuna flani na flani ambae ametenda madhambi mengi, na amefika tu mwisho wa mkusanyiko. Allah subhaana wata'ala atasema, "wafunike watu wote wa mkusanyiko huo (pamoja na yeye) kwa rehema zangu, kwa sababu watu katika mkusanyiko huu ni kama kwamba hakuna mtu yoyote anayejiunga nao atakuwa na bahati mbaya ya kunyimwa rehema zangu."
Soma Zaidi »