Zubair (Radhiya Allaahu ‘anhu) Akiwapa Watoto Zake Majina Baada Ya Mashahidi Wa Maswahaabah (Radhiya Allaahu ‘anhum)

Zubair (Radhiya Allaahu ‘anhu) aliwahi kutaja:

“Hakika Talha bin ‘Ubaidillah (Radhiya Allaahu ‘anhu) anatoa majina ya Ambiyaa (‘Alaihimus salaam) kwa watoto zake, ambapo anajua kwamba hakutokuwa Nabii atakayekuja baada ya Nabii Muhammad (Sallallahu ‘alaihi wasallam). Kisha Zubair (Radhiya Allaahu ‘anhu) akasema: “Natoa majina ya mashahidi (wa Maswahaabah) kwa wanangu ili wanangu wapate kubarikiwa kufa kishahidi.”

Hivyo basi, Zubair (Radhiya Allaahu ‘anhu) alimwita mtoto wake ‘Abdullah baada ya ‘Abdullah bin Jahsh (Radhiyallahu ‘anhu) (aliyeuawa kishahidi katika vita vya Uhud).

Alimwita mwanawe Mundhir baada Mundhir bin ‘Amr (Radhiyallahu ‘anhu) (aliyeuawa kishahidi katika Biru Maoonah).

Alimwita mwanawe ‘Urwah baada ya ‘Urwah bin Mas’uud (Radhiya Allaahu ‘anhu) (aliyeuawa na watu wake alipowalingania kwenye Uislamu).

Alimwita mwanawe Hamzah baada ya Hamza bin ‘Abdil Muttalib (Radhiya Allaahu ‘anhu) (ambaye aliuawa kishahidi katika vita vya Uhud).

Alimwita mwanawe Ja’far baada ya Ja’far bin Abi Thaalib (Radhiya Allaahu ‘anhu) (aliyeuawa kishahidi katika vita vya Mu’tah).

Alimwita mwanawe Mus‘ab baada ya Mus‘ab bin ‘Umair (Radhiya Allaahu ‘anhu) (aliyeuawa kishahidi katika vita vya Uhud).

Alimwita mwanawe ‘Ubaidah baada ya ‘Ubaidah bin Haarith (Radhiya Allaahu ‘anhu) (aliyeuawa kishahidi katika vita vya Badr).

Alimwita mwanawe Khaalid baada ya Khaalid bin Sa‘id (Radhiya Allaahu ‘anhu) (aliyeuawa kishahidi katika vita vya Marjus Safar au Ajnadin).

Alimwita mwanawe ‘Amr baada ya ‘Amr bin Said bin ‘Aas (Radhiya Allaahu ‘anhuma) ambaye aliuawa katika Vita vya Yarmuk. (Tabaqaat ibn Sa’d 3/74)

About admin

Check Also

Abu Ubaidah (Radhiya Allaahu ‘anhu) Apoteza Meno Yake Katika Vita Vya Uhud

Wakati wa vita vya Uhud, Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) alishambuliwa na maadui na viungo viwili …