Sunnah Na Adabu Za Kuwatembelea Marehemu 3

9. Ni makrooh kwa mtu kufanya ta’ziya kwa mara ya pili wakati tayari ameshafanya ta’ziya kabla.

10. Ni vyema kufanya ta’ziya baada ya kuzika. Hata hivyo, inaruhusiwa kufanya ta’ziya kabla ya kuzikwa.

11. Ikiwa mtu hawezi kwenda kufanya ta’ziya kutokana na dharura, basi anaweza kuandika barua au kutuma message kwa familia ya marehemu.

12. Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam) aliwafariji wafiwa kwa maneno yafuatayo:

إِنَّ لِلّٰهِ مَا أَخَذَ وَلَهُ مَا أَعْطٰى وَكُلٌّ إِلٰى أَجَلٍ مُسَمًّى فَلْتَصْبِرْ وَلْتَحْتَسِبْ

Anachokichukua ni cha Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’alah), na ni Chake Pekee Anachotoa. Kila kitu kinabakia mpaka muda uliowekwa (baada ya hapo kitaondolewa hapa duniani). Basi kuwa na subira na tarajia malipo kutoka kwa AllahTa’ala.

13. Haijuzu kwenda nyumbani kwa kafiri aliyefariki kufanya ta’ziya wakati shughuli za mazishi zikiendelea. Lakini, katika kukutana na jirani kafiri au kafiri mwingine yoyote ambaye amefiwa na mwanafamilia kama mtoto, mtu anaweza kumfariji kwa maneno yafuatayo:

أَخْلَفَ اللَّهُ عَلَيْكَ خَيْرًا مِّنْهُ وَأَصْلَحَكَ

Allah Ta’ala Akujaalie kilicho bora zaidi (akupe tawfeeq ya kusilimu) badala ya mtu uliyempoteza, na Allah Ta‘ala aiboreshe hali yako.

AUD-20240807-WA0001

About admin

Check Also

Fadhila Za Kutoa Salaam

Fadhila Ya Kutoa Salaam Wakwanza Abdullah bin Mas’uud (Radhiya Allaahu ‘anhu) anasimulia kwamba Mtume (Sallallahu …