Katika tukio la Khaibar, baada ya Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) kukabidhi bendera ya Uislamu kwa Ali (radhiya allaahu anhu), Ali (radhiyallahu anhu) aliliongoza jeshi la Maswahaabah (radhiyallahu anhu) hadi kwenye ngome ya Qamoos. Walipokaribia ngome, shujaa mmoja wa kiyahudi, jina lake Marhab, alitoka ili kuwapinga (waislamu). Marhab alikuwa shujaa maarufu …
Soma Zaidi »Hofu Ya Ali (radhiya allaahu ‘anhu) Na Akhera
Kumail ibn Ziyad (rahimahullah) anaripoti yafuatayo: Wakati mmoja, nilifuatana na Ali (radhiya allaahu ‘anhu) alipokuwa akitoka katika mji wa Kufah na kuelekea Jabbaan (kijiji nje ya Kufah). Alipofika Jabbaan, Ali (radhiya allaahu ‘anhu) aligeuka kuelekea makaburini na akaita, “Enyi wakazi wa makaburini! Enyi watu ambao miili yenu imeoza! Enyi watu …
Soma Zaidi »Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) Amemchagua Ali (radhiya allaahu ‘anhu) Kuisimamia Madinah Munawwarah
Katika tukio la Vita vya Tabook, wakati Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam) alipokuwa anaondoka kutoka Madinah Munawwarah, alimchagua Ali (radhiya allaahu ‘anhu) kusimamia mambo ya Madinah Munawwarah akiwa hayupo. Kwa hiyo, kwa maelekezo ya Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam), Ali (radhiya allaahu ‘anhu) hakutoka na jeshi, bali alibakia Madinah Munawwarah. Baada ya …
Soma Zaidi »Ushujaa wa Ali (radhiya allaahu ‘anhu)
Wakati wa Vita vya Uhud, Ali (radhiyallahu ‘anhu) alionyesha ujasiri na ushujaa wa hali ya juu katika kupigana na maadui. Hivyo, yeye binafsi alihusika kuwaua viongozi wanne wa Maquraishi, miongoni mwao akiwa ni Talhah bin Abi Talhah. Baada ya vita, alimkabidhi upanga wake kwa mke wake mheshimiwa, Faatimah (radhiya allaahu …
Soma Zaidi »Mapenzi ya Ali (radhiya allaahu ‘anhu) kwa Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam)
Wakati mmoja, Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam) alikuwa hana chakula na kuhisi njaa. Wakati Ali (radhiya allaahu ‘anhu) alipopata habari kwamba Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam) alikuwa akipatwa na njaa, mara moja moyo wake ulijaa na wasiwasi. Hayo yalikuwa mapenzi yake kwa Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam) kiasi kwamba hakuweza kupumzika huku akijua …
Soma Zaidi »Dua ya Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) kwa Ali (radhiya allaahu ‘anhu) wakati wa Kumtuma kwenda Yemen
Ali (radhiya allaahu ‘anhu) anaripoti: Rasulullah (sallallahu ‘alahi wasallam) alinituma kama waziri wake kwenda Yemen. Kabla ya kuondoka, nilimwambia, “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu (sallallahu ‘alaihi wasallam)! Unanipeleka kwa watu ambao ni wakubwa kuliko mimi. Zaidi ya hayo, mimi ni kijana na sina ufahamu wowote katika uwanja wa Qadhaa (mambo …
Soma Zaidi »Kununua Ardhi kwa ajili ya Upanuzi wa Masjid-ul-Haram
Wakati mmoja, Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) alimwendea mtu fulani huko Makka Mukarramah na kumwambia, “Ewe fulani! Je, utaniuzia nyumba yako, ili nipanue eneo la msikiti karibu na Al-Ka’ba, na kwa malipo ya tendo hili jema, nitakudhaminia kasri katika Jannah (yaani zaidi ya pesa utakazopokea ya nyumba hii)?” Yule mtu akajibu, …
Soma Zaidi »Kuandaa Vifaa katika Msafara wa Tabook
Abdur Rahmaan bin Khabbaab (radhiya allaahu ‘anhu) anasimulia yafuatayo: Nilikuwepo wakati Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) alipokuwa akiwahimiza Maswahabah (radhiyallahu ‘anhum) kuliandaa jeshi na kuchangia katika msafara wa Tabook. Katika tukio hilo, ‘Uthmaan (radhiya allaahu ‘anhu) alisimama na kusema, “Ewe Mtume wa Allah (Sallallahu ‘alaihi wasallam)! Ninajitolea kuchangia ngamia mia moja …
Soma Zaidi »Wasiwasi Wa Kuulizwa Akhera
Wakati mmoja, ‘Uthmaan (radhiya allaahu ‘anhu) aliingia kwenye nyumba ya mnyama na akamkuta mtumwa wake akimlisha chakula ngamia. Katika kukagua malisho, ‘Uthmaan (radhiya allaahu ‘anhu) hakufurahishwa na jinsi mtumwa wake alivyoitayarisha chakula na hivyo akamfinya sikio lake. Baada ya muda kidogo na kuchunguza matendo yake, ‘Uthmaan (radhiya allaahu ‘anhu) aliingiwa …
Soma Zaidi »Fadhila Kumi Maalum Za ‘Uthmaan (radhiya allaahu ‘anhu)
Abu Thowr (rahimahullah) anasimulia kwamba siku moja alikuja kwa ‘Uthmaan (radhiya allahu ‘anhu) na kumsikia akitaja yafuatayo wakati ukosoaji usio sahihi ulipokuwa ukitolewa dhidi yake. Alisema: Kuna mema kumi ambayo nimeyalinda kwa Allah Taala na kwa kila amali natarajia kupata malipo ya Akhera; 1) Nilikuwa mtu wa nne kusilimu. 2) …
Soma Zaidi »