Kujiepusha Kwa Abu Ubaidah (Radhiya Allaahu ‘anhu) Na Utajiri wa Dunia

Wakati Umar (Radhiya Allaahu ‘anhu) alipotoka Madinah Munawwarah kwenda Baitul Muqaddas ili kuliteka, alisimama Shaam kukutana na Maswahaba waliokuwa wakiishi huko. Maswahabah (Radhiya Allaahu ‘anhum) waliokuwa wakiishi Shaam na kutawala Shaam walipokuja kukutana naye, akawauliza, “Ndugu yangu yuko wapi?”maswahaabah (Radhiya Allaahu ‘anhu) wakauliza: “Unamtaja nani?” Umar (Radhiya Allaahu ‘anhu) akajibu, “Abu ‘Ubaidah (Radhiya Allaahu ‘anhu).”

Maswahaabah (Radhiya Allaahu ‘anhum) walimjulisha kwamba Abu Ubaidah (Radhiya Allaahu ‘anhu) hivi karibuni alikuwa anakuja kukutana naye. Baada ya muda mfupi, Abu ‘Ubaidah (Radhiya Allaahu ‘anhu) alifika akiwa amepanda ngamia wa kawaida.

Wakati Abu Ubaidah (Radhiya Allaahu ‘anhu) alipokutana na Umar (Radhiya Allaahu ‘anhu), Umar (radhiyallahu ‘anhu) alionyesha furaha kubwa na mara moja akamkumbatia. Umar (Radhiya Allaahu ‘anhu) baada ya hapo alitoa khutbah kwa Swahaabah (Radhiya Allaahu ‘anhu) na wote waliokuwepo pale. (Hilyatul Awliyaa juzuu ya 1, pg 146 na Kitaabuz Zuhd libnil Mubaarak [rahimahullah])

Wakati huo, Maswahabah (Radhiya Allaahu ‘anhum) walimwalika Umar (Radhiya Allaahu ‘anhu) majumbani mwao, lakini Abu Ubaidah (Radhiyallahu ‘anhu) hakumwalika Umar (Radhiya Allaahu ‘anhu) nyumbani kwake kwa ssbabu wakati huo hakuwa na chochote cha kumkirimu Umar (radhiyallahu ‘anhu).

Kupitia uhusiano wa karibu aliokuwa nao Umar (Radhiya Allaahu ‘anhu) naye, Umar (Radhiya Allaahu ‘anhu) alimwambia akisema, “Ewe Abu Ubaidah! (Kutoka kwa maswahaabah) kila kiongozi wa jeshi ameniita nyumbani kwake ispokuwa wewe.” Abu Ubaidah (Radhiya Allaahu ‘anhu) akamwambia: “Ewe Ameerul Mu-mineen! itakutoa machozi.”

Hata hivyo, Umar (Radhiya Allaahu ‘anhu) alitaka kutembelea nyumba ya Sahaabi huyu mkubwa, kwa hiyo, Abu Ubaidah (Radhiya Allaahu ‘anhu) alimkaribisha Umar (Radhiya Allaahu ‘anhu) nyumbani kwake kama mgeni wake.

Wakati Umar (Radhiya Allaahu ‘anhu) alipoingia nyumbani kwake, alishangaa kuona kwamba vitu alivyokuwa navyo ni vipande vya mkate mkavu, mfuko wa maji, upanga, ngao, mfuko wa tandiko, na blanketi ya kutandika ambayo pia aliitumia kama tandiko na mto wa kulala usiku.

Umar (Radhiya Allaahu ‘anhu) alipoona hivyo, alianza kulia na kisha akamkumbatia Abu Ubaidah (Radhiya Allaahu ‘anhu) akisema, “Hakika wewe ni ndugu yangu. Naona kwamba Maswahaba wote ambao nimekutana nao, ulimwengu umewaathiri (kwa kiasi fulani, kama wamechukua sehemu ya vitu vya kidunia vya kunufaika navyo) ispokuwa wewe” Abu Ubaidah (Radhiya Allaahu ‘anhu) akajibu akisema, “Je, sikukuambia, ewe Amirul-Mumineen, kwamba ukizuru nyumbani kwangu utatokwa na machozi (kwa ajili hautokuta utajiri wa dunia ndani yake)?

Kwa mujibu wa riwaya moja, Umar (Radhiya Allaahu ‘anhu) kisha akamwambia, “Kwa nini usiweke angalau baadhi ya bidhaa za dunia au vitu ili ufaidike navyo?”

Hata hivyo, Hadhrat Abu Ubaidah (Radhiya Allaahu ‘anhu) akajibu akisema, “Ewe Ameerul Mumineen! Kiasi hiki kinatosha kwa safari yangu katika ulimwengu huu hadi nifike kaburini mwangu.”

About admin

Check Also

Matendo Ya Abu Ubaidah (Radhiya Allaahu ‘anhu) Yanwafikiana na Quran Majeed

Katika vita vya Badr, baba yake Abu Ubaidah aliendelea kumfuatilia akijaribu kumuua. Hata hivyo, yeye …