Sunnat Na Adabu Za Kuamkiana (Kutoa Salaam) 3

8. Unapojibu salamu, inajuzu kwako kujibu kwa salamu ambayo ni sawa na salamu iliyopokelewa. Lakini, ukijibu kwa salaam ndefu zaidi itakuwa bora na yenye thawabu zaidi. Kwa mfano, kama ulisalimiwa kwa maneno “Assalaamu alaikum”, basi unaweza kujibu kwa kusema “Wa alaikumus salaam”. Hata hivyo, ni bora na yenye thawabu zaidi kwako kusema “Wa alaikumus salaam wa rahmatullah” au “Wa alaikumus salaam wa rahmatullahi wa barakaatuhu.”

Allah Ta’ala ametaja ndani ya Qur-aan Majeed, “Na mtakapokuwa mmesalimiwa kwa salamu, basi jibu salamu kwa salamu bora kuliko hiyo au rudisha (rudisha salamu kama uliosalimiwa).[1]

9. Maneno ya salaam yanaishia na “Wa barakaatuhu”. Mtu asipaswi kuongeza maneno mengine baada ya “Wa barakaatuhu”.

Muhammad bin Amr bin Ataa’ (rahimahullah) anasimulia: Wakati mmoja, nilikaa pamoja na Abdullah bin Abbaas (radhiyallahu anhuma) pindi mtu mmoja kutoka Yemen alipoingia kwenye mkusanyiko na akatoa salaam akisema: “Assalaamu alaikum wa rahmatullahi wa barakatuhu,” kisha akaongeza maneno machache kwenye salamu. Wakati huo, Abdullah bin Abbaas alikuwa amepoteza uwezo wa kuona, hivyo akauliza, “Mtu huyu ni nani?” Watu wake wakasema: “Huyu ndiye yule mtu kutoka Yemen ambaye anakuwa akihudhuria mikusanyiko wako.” Walimuelezea hadi Abdullah bin Abbaas (radhiyallahu anhuma) akamtambua. Abdullah bin Abbaas (radhiyallahu anhuma) kisha akasema, “Salaam inaisha na barakah (yaani kwa kusema wabaraakatuhu).”[2]

10. Unapojibu salamu ya mtu, jibu salamu kwa maneno na si kwa ishara tu ya mkono au kutikisa kichwa.


[1] سورة النساء: 86

[2] المؤطا للإمام محمد، صـ 385

About admin

Check Also

Sunnat Na Adabu Za Kuamkiana (Kutoa Salaam) 6

18. Ukiingia kwenye mkusanyiko wenye mazungumzo au majadiliano ya Dini inafanyika, hupaswi kutoa salaam kwa …