Umar (Radhiya Allaahu ‘anhu) Akimuamini Abu Ubaidah (Radhiya Allaahu ‘anhu)

Umar (Radhiya Allaahu ‘anhu) aliwahi kufika kwenye mipaka ya Shaam (Syria) alipojilishwa habari ya thauni iliyowapata watu wa Shamu.

Umar (Radhiya Allaahu ‘anhu) amesema: “kama kifo kitanifikia wakati Abu Ubaidah bin Jarrah (Radhiya Allaahu ‘anhu) bado yupo hai, basi nitamchagua yeye kuwa khalifah baada yangu, na ikibidi Allah Ta’ala aniulize, ‘Kwa nini ulimchagua Abu Ubaidah (Radhiya Allaahu ‘anhu) kuwa khalifah na kutawala Waislamu (baada yako)?’, nitamwambia Allah Ta’ala sababu ya mimi kumchagua ni kwamba niliwahi kumsikia Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) akitaja, “Kila Nabii alikuwa na mfuasi maalumu (kwenye umma wake) na mfuasi wangu maalumu (juu ya umma wangu) ni Abu Ubaidah bin Jarraah (Radhiya Allaahu ‘anhu).” (Musnad Ahmad #108)

Imepokelewa kwamba Wakati Umar (Radhiya Allaahu ‘anhu) alipokaribia kuaga dunia, aliunda kundi la Maswahaabah sita (Radhiyallahu ‘anhum) na akaagiza kwamba waamue wao kwa wao ni nani atachaguliwa kuwa khaleefah baada yake.

Wakati huo, Umar (Radhiya Allaahu ‘anhu) alisema, “Lau Abu Ubaidah angekuwa hai leo, kwa hakika ningemchagua yeye kuwa khaleefah (wa Waislamu). (Tafsir Ibn Katheer 8/54)

About admin

Check Also

Tamaa Ya Umar (Radhiya Allaahu ‘anhu) Kubarikiwa Na Chumba Kilichojaa Na Watu Kama Abu Ubaidah (Radhiya Allaahu ‘anhu)

Umar (Radhiya Allaahu ‘anhu) wakati fulani alikua amekaa pamoja na kundi la watu alipokuwa akiwahutubia …