Katika vita vya Badr, baba yake Abu Ubaidah aliendelea kumfuatilia akijaribu kumuua. Hata hivyo, yeye aliendelea kumkwepa baba yake ili asikutani naye na kumuua.
Lakini, baba yake alipong’ang’ania na mwisho wakakutana na hapakuwa na njia nyingine ya kuokoa maisha ya baba yake isipokua kumuua baba yake, alikwenda mbele na kumuua.
Ilikuwa ni katika tukio hili ambapo Allah Ta’ala aliteremsha aya ifuatayo:
لَّا تَجِدُ قَوْمًا يُؤْمِنُونَ بِاللَّهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ يُوَادُّونَ مَنْ حَادَّ اللَّهَ وَرَسُولَهُ وَلَوْ كَانُوا آبَاءَهُمْ أَوْ أَبْنَاءَهُمْ أَوْ إِخْوَانَهُمْ أَوْ عَشِيرَتَهُمْ ۚ
“Hutawakuta wale wanaomuamini Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’alah) na Akhera wanawapenda wale wanaompinga Allah Ta’ala na Mtume Wake (Sallallahu alaihi wasallam), ijapokuwa watu hao ni baba zao, watoto zao, ndugu zao, au (watu wao kutoka kwenye) kabila lao.” (Surah Mujaadalah v22) Majma’uz Zawaaid #14906