Fadhila Za Kutoa Salaam

Fadhila Ya Kutoa Salaam Wakwanza

Abdullah bin Mas’uud (Radhiya Allaahu ‘anhu) anasimulia kwamba Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) alisema, “Mwenye kutoa salaam wakwanza hana kiburi.”

Jinsi ya Kuunda Upendo Kati Yetu

Imepokewa kutoka kwa Abu Huraira (radhiyallahu ‘anhu) kwamba Mtume (sallallahu alaihi wasallam) amesema: “Hamtaingia Peponi mpaka mlete Imaan, na huwezi kupata Imaan kamili mpaka mmiliki upendo baina yenu. Je, niwaonyeshe jinsi ya kuwa na upendo kati yenu? Fanyeni salaam kuwa ni jambo la kawaida baina yenu (wakati wa kukutana).”

Kitendo Cha Thawabu Kubwa Ndani Ya Uislamu

Abdullah bin Amr (Radhiyallahu ‘anhuma) anaripoti kwamba mtu mmoja aliwahi kumuuliza Mtume (sallallahu alaihi wasallam), “Ni kipengele gani na adabu gani ya Uislamu ni ya kusifiwa sana na yenye thawabu?” Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) akajibu: “Kulisha viumbe na kuwatolea salamu watu, ukiwa unawajua au huwajui.”

Kuleta Baraka Nyumbani Kwako

Anas (Radhiyallahu anhu) anasema: Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) aliniambia, “Ewe mwanangu kipenzi! Unapoingia nyumbani kwako, salimia familia yako kwa kutoa salaam. Hii itakuwa njia ya wewe na familia yako kupata baraka.”


[1] شعب الإيمان للبيهقي، الرقم: 8407، وقال المناوي في فيض القدير، الرقم: 3191، وفيه أبو الأحوص قال ابن معين: ليس بشيء وأورده الذهبي في الضعفاء

[2] صحيح مسلم، الرقم: 54

[3] صحيح البخاري ، الرقم: 12

[4] سنن الترمذي، الرقم: 2698، وقال: هذا حديث حسن غريب

About admin

Check Also

Sunnah Na Adabu Za Kuwatembelea Marehemu 4

14. Wasaidie waliofiwa kwa kuwapelekea chakula nyumbani kwao. Mtume (Sallallahu ‘alaihi wasallam) amewafundisha Maswahaba (radhiyallahu …