Abu Ubaidah (Radhiya Allaahu ‘anhu) Apoteza Meno Yake Katika Vita Vya Uhud

Wakati wa vita vya Uhud, Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) alishambuliwa na maadui na viungo viwili vya kofia yake ya chuma vikapenya kwenye uso wake wa baraka.

Abu Bakr Siddiq (Radhiya Allaahu ‘anhu) na Abu Ubaidah (Radhiya Allaahu ‘anhu) mara moja wakakimbia kwenda kumsaidia Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam). Abu Ubaidah (Radhiya Allaahu ‘anhu) alianza kung’oa viungo kwa meno yake. Kufikia wakati kiungo kimoja kilitolewa, alikuwa amepoteza jino limoja. Hakujutia kupotea kwa jino lake, akatumia tena meno yake kung’oa kiungo kingine pia. Alifanikiwa kukiondoa kiungo kingine, hata hivyo katika harakati hizo, alipoteza jino lingine.

Viungo vilipotolewa, damu ilianza kutoka kwenye mwili wa Mtume (Sallallahu alaihi wasallam). Malik bin Sinaan (Radhiya Allaahu ‘anhu), baba yake na Abu Said Khudri (Radhiyallahu ‘anhu), akaanza kulamba damu kwa midomo yake. Kwa hili, Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) alisema, “Moto wa Jahannam hauwezi kumgusa mtu ambaye damu yangu imechanganyika na yake.”
(Musnad Abi Dawood Tayaalisi #6 & Fathul Baari 7/366)

About admin

Check Also

Nafasi Ya Juu Ya Abu Ubaidah (Radhiya Allaahu ‘anhu) Mbele Ya Abu Bakr (Radhiya Allaahu ‘anhu)

Baada ya kufariki kwa Mtume (Sallallahu alaihi wasallam), Ma answaar walikuwa wamekusanyika huko Thaqifah Bani …