Salaam

Salaam ni kumsalimia muislamu. Kama vile Uislamu unavyosimamia amani, maamkizi ya Uislamu ni salamu ya amani na kueneza ujumbe ya amani. Salaam ni moja ya mila za kiislamu ambazo ni sifa ya Muislamu na umuhimu wake umesisitizwa sana katika hadith ya mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam).

Abdullah bin Salaam (radhiyallahu ‘anhu) anaripoti: Wakati Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) alihamia Madinah Tayyibah, watu wa Madinah Tayyibah walikimbilia kumpokea. Nilimsikia mtu akiita mara tatu, “Mtume wa Mwenyezi Mungu amefika! Mjumbe wa Mwenyezi Mungu amefika! Mtume wa Mwenyezi Mungu amefika!”

Pia nilienda na watu kuchunguza mimi mwenyewe (utu ambao watu walidai kuwa ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, ingawa nilikuwa bado sijasilimu mpaka hapo). Mara tu macho yangu yalipoangukia uso wa Mtume (sallallahu alaihi wasallam) ndipo nilikuwa na uhakika kwamba uso huu hauwezi kuwa uso wa mwongo.

Maneno ya kwanza niliyomsikia akiyasema wakati akiwahutubia watu (kwenye tukio hilo la furaha) yalikuwa, “Enyi watu! Toeni salaam baina yenu (Ifanye salaam iwe ya kawaida baina yenu wakati wa kukutana), lisheni viumbe, na suluhisheni kati ya familia, na simameni katika Swalaah wakati wa usiku wakati watu wamelala, kwa njia hii utabarikiwa kuingia peponi na amani.’”

Katika Hadith, Mtume (sallallahu alaihi wasallam) ameeleza kwamba kutoa salaam ni njia ya kujenga mapenzi ya umoja katika Ummah, na vilevile ni njia ya kuingia Jannah.

Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) amesema: “Hamtaingia Peponi mpaka mlete Imaan, na hamwezi kupata Imaan kamili mpaka muwe na mapenzi baina yenu. Je! nikuonyesheni njia ambayo mtahimizana kupendana? Toeni salaam baina yenu (wakati wa kukutana).”

Kumsalimia Muislamu ni miongoni mwa haki sita za ujumla ambazo kila mtu anadaiwa na ndugu yake Muislamu.

1) Anamuombea dua kwamba Allah Ta’ala abaki kwenye amani, kwasababu salaam ni maamkizi ya amani.

2) Anamkumbusha kuwa Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’alah) yupo pamoja naye na anamtazama kila wakati, kwa sababu ‘Salaam’ ni jina la Allah Ta’ala.

3) Anamjulisha kuwa anapokuwa amemsalimia na salamu ya amani, hakika yeye ni mtakia wema na hatomdhuru kwa lolote (si kwa maneno, wala kimwili wala kwa njia nyingine yoyote).

About admin

Check Also

Sunnah Na Adabu Za Kuwatembelea Marehemu 4

14. Wasaidie waliofiwa kwa kuwapelekea chakula nyumbani kwao. Mtume (Sallallahu ‘alaihi wasallam) amewafundisha Maswahaba (radhiyallahu …