Tamaa Ya Umar (Radhiya Allaahu ‘anhu) Kubarikiwa Na Chumba Kilichojaa Na Watu Kama Abu Ubaidah (Radhiya Allaahu ‘anhu)

Umar (Radhiya Allaahu ‘anhu) wakati fulani alikua amekaa pamoja na kundi la watu alipokuwa akiwahutubia na kuwauliza swali lifuatalo, “Niambieni nyinyi watu mnatamani kitu gani!”

Mtu mmoja alisema: “mimi natamani chumba hiki kizima kijazwe na dirham (sarafu za fedha) na nizitoe zote katika Njia ya Allah Ta’ala.”

Umar (Radhiya Allaahu ‘anhu) kisha akawahutubia watu na kuwauliza kwa mara ya pili, “Niambieni mnatamani kitu gani!”

Mtu mwingine alisema: “Tamaa niliyo nayo ni kwamba chumba hiki kizima kijazwe na sarafu za dhahabu na nizitoe zote katika njia ya Allah Ta’ala.”

Kwa mara nyingine tena Umar (Radhiya Allaahu ‘anhu) aliwahutubia watu na kuuliza swali lile lile, “Niambieni mna tamani kitu gani!

Mtu wa tatu akasema: “tamaa niliyo nayo ni kwamba chumba hiki chote kijazwe na mawe ya dhahabu na nivitumie vyote katika njia ya Allah Ta’ala.

Umar (Radhiya Allaahu ‘anhu) aliuliza swali lile kwa mara ya nne akiuliza kama kuna mtu yoyote mwingine alikuwa na tamani kitu chochote, lakini walijibu kwamba hawakutamani kitu kingine chochote.

Hapo, Umar (Radhiya Allaahu ‘anhu) akaeleza matamanio yake akisema: “Hamu niliyo nayo ni kwamba chumba hiki kijazwe na watu kama Abu Ubaidah, Mu’aadh bin Jabal na Huzaifah bin Yamaan (Radhiya Allaahu ‘anhum). ili niweze kuwatumia kila moja katika kumtii Allah Taala (yaani. Ningeweza kuwatumia kufanya kazi ya Dini na kueneza Dini ulimwenguni). (At-Taareekhus Sagheer juzuu ya 1, uk. 79)

About admin

Check Also

Abu Ubaidah (Radhiya Allaahu ‘anhu) Apoteza Meno Yake Katika Vita Vya Uhud

Wakati wa vita vya Uhud, Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) alishambuliwa na maadui na viungo viwili …