Sunnah Na Adabu Za Kuwatembelea Marehemu 4

14. Wasaidie waliofiwa kwa kuwapelekea chakula nyumbani kwao. Mtume (Sallallahu ‘alaihi wasallam) amewafundisha Maswahaba (radhiyallahu ‘anhum) kuonesha huruma kwa wafiwa na kuwasaidia wakati wa huzuni zao. Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam) aliwahimiza Maswahaba (Radhiya Allaahu ‘anhum) kuandaa chakula na kupeleka kwa ajili ya familia, kwa sababu kupata msiba huu itakuwa vigumu kwao kutekeleza mahitaji yao.

Abdullah bin Ja’far (Radhiya Allaahu ‘anhu) anasimulia, “Wakati habari za kufariki kwa Ja’far (Radhiya Allaahu ‘anhu) ilipofika (yaani habari za kifo chake cha kishahidi katika Vita vya Muutah), Mtume (Sallallahu ‘alaihi wasallam) aliwaambia Maswahabah (Radhiya Allaahu ‘anhu), ‘Waandalieni familia ya Ja’far (Radhiya Allaahu ‘anhu) chakula, kwa sababu msiba umewasibu ambao umewashughulisha (kutekeleza haja zao).)’”

15. Shari’ah haijabainisha aina yoyote maalum au rangi ya nguo inayopaswa kuvaliwa na mfiwa.

16. Desturi ya wageni wanaokuja siku ya tatu, saba, siku ya kumi na siku ya arobaini kwenye “khitma au kukhitimu” n.k. ni upotovu na bid’aa na inapaswa kuachwa.

17. Chakula haipaswi kutolewa nyumbani kwa marehemu wale wanaokuja kufanya ta’ziya. Kuhudumia chakula nyumbani ni kitendo cha upotovu na bid’aa.

18. Haijuzu kumwajiri mtu kusoma Quran Majeed na kufikisha malipo kwa marehemu.


 

About admin

Check Also

Fadhila za Jumu’ah

Kusamehewa Madhambi Kwa Kuswali Jumu’ah Imepokewa kutoka kwa Abu Hurairah (radhiyallahu anhu) kwamba Mtume (Sallallahu …