Tukio La Mchamungu, Abdullah Bin Marzooq

Abdullah bin Marzooq (rahimahullah) alikuwa mja mchamungu wa Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’aalah)na alikuwa katika zama za Muhadditheen wakubwa, Sufyaan bin Uyainah na Fudhail bin Iyaadh (rahimahumullah).

Mwanzoni, alikuwa na mwelekeo wakupenda dunia na hakujitolea kwenye mambo ya dini. Hata hivyo, Allah Ta‘ala akambariki na tawfeeq ya kutubia na kurekebisha maisha yake. Ifuatayo ni tukio ya kutubu kwake:

Wakati fulani, Abdullah bin Marzooq (rahimahullah) alikuwa amezama katika ubatili, akinywa pombe na kusikiliza miziki. Wakati akijishughulisha na madhambi haya, Swalaah zake za Dhuhr, Asr na Maghrib zilikuwa zikimpita.

Kila wakati wa Swalaah ulipoingia, mmoja wa vijakazi wake alimjia na kumkumbusha kuswali. Lakini, kwa sababu ya yeye kujishughulisha na unywaji wa pombe na burudani, hakuzingatia ukumbusho wake.

Hatimaye, wakati wa Swalaah ya isha pia ulikuwa umepita na usiku ulipokwisha, mjakazi wake alichukua makaa ya moto na kuyaweka juu ya mguu wake.

Makaa ya moto ilipogusa mguu wake, alipiga kelele kwa uchungu na kumuuliza, “Unafanya nini! Yule mjakazi akajibu, “Usipoweza kustahimili makaa ya moto linalowaka katika dunia hii, basi utaustahimilije moto wa
Jahannum?”

Aliposikia ushauri huo kutoka kwa kijakazi wake, alitokwa na machozi mara moja. Hii ilikuwa hatua ya mabadiliko katika maisha yake.

Hivyo alitubia kwa Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’alah) na akalipiza Swalah zote ambazo alikuwa amezikosa. Kisha akarekebisha maisha yake na akaacha maisha yake ya dhambi. Alijitolea mali yake katika njia ya Allah Ta’ala na akaanza kuishi maisha ya urahisi, akitosheleza na mali kidogo ya dunia.

Baada ya kuyarekebisha maisha yake, katika tukio moja, Sufyaan bin Uyainah (rahimahullah) na Fudhail bin Iyadh (rahimahullah) walimtembelea. Walikuwa wamemkuta akiishi maisha ya urahisi kabisa ya kuendana na Sunnah.

Sufyaan (rahimahullah) akamuuliza, “Imetajwa katika Hadithi kwamba mtu anapotoa kitu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’aalah), basi Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’aala) Humruzuku kitu kilicho bora zaidi. Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’aalah) amekupa wewe nini kwenye nafasi ya yote ulioyaacha?”

Abdullah bin Marzouq (rahimahullah) akajibu, “Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’aalah) amenijaalia furaha ya kweli na kutosheka kwa moyo.”

Kumkumbuka (Kumdhukuru) Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’alah)- Chakula cha Nafsi.

Kila mtu anatafuta furaha ya kweli na kutosheka kwa moyo. Baadhi ya watu huitafuta katika mali, nyumba za kifahari na magari. Wengine huitafuta sehemu za bahari, vivutio vya watalii na vituo vya burudani. Wengine huitafute katika michezo, na burudani.

Hata hivyo, Allah Ta‘ala ameweka furaha ya kweli na kutosheka kwa moyo katika mapenzi na ukumbusho Wake. Mapenzi ya Allah Ta’ala ndio chanzo cha furaha ya kweli na kutosheka kwa moyo.

Katika Qur-aan Majeed, Allah Ta’ala Anasema:

أَلَا بِذِكْرِ اللَّهِ تَطْمَئِنُّ الْقُلُوبُ ‎﴿٢٨﴾‏

Tazama! Ni kwa kumkumbuka (kumdhukuru) Allah Ta’ala pekee nyoyo hupata kuridhika (na furaha).

Mtu anapotafakari juu ya mwanadamu, anatambua kuwa Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’aalah) amemuumba kwa vipimo viwili. Ya kwanza ni mwili wake wa kimwili ambao unajumuisha umbo lake la nje, na la pili ni mwili wake wa kiroho ambao unajumuisha nafsi yake (rooh).

Ama mwili wa mwanadamu, basi Allah Ta’ala aliuumba kwa udongo. Kwa hiyo, mwili unahitaji vitu vya kimwili vya ulimwengu huu (k.m. chakula, vinywaji, mavazi, nyumba, gari, n.k.) kwa ajili ya riziki yake, utimizo na kuridhika.

Ama mwili wa kiroho wa mwanadamu (Rooh), basi kwa Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’alah) hakuiumba kutoka kwenye ardhi, bali ameiumba Mbinguni, riziki yake, utulivu wake na kutosheka kwake hupatikana kwa vitendo vya mbinguni.

Vitendo hivi vya mbinguni vinarejelea amri za shari’ah (k.m. Swalaah, zakaah, saumu, n.k.) ambazo hutumika kama chakula cha kiroho kwa nafsi.

Mtu anaposwali, akafunga, akatoa sadaqah, anasoma Quran Majeed na anajihusisha na vitendo vingine vya ibada, basi nafsi yake inapokea chakula cha kiroho ambacho Allah Ta’ala ameumba kama riziki yake.

Kwa hivyo, nafsi yake (roho yake) imeangaziwa na nuru ya shari’ah na anaona hisia ya furaha na utulivu.

Kinyume chake, mtu anapojihusisha na matendo maovu na madhambi kama vile kutumia macho vibaya, kula haramu, kuiba,
kufanya zinaa, kudhulumu watu, kufanya matendo mabaya, kucheza kamari n.k basi moyo wake unapoteza nuru ya Imaan na
imefunikwa na giza la madhambi.

Matokeo yake, anaona hali ya taabu na nafsi inakosa furaha na utulivu wa kweli.

Mfumo Wa Kutosheka Kwa Moyo

Mchamungu mkubwa wa wakati huu,Sheikh Ashraf Ali Thanwi (rahimahullah) aliwahi kutaja yafuatayo:

Kupata furaha ya kweli hakutegemei kuwa na vitu vingi vya utajiri. Badala yake, kupata furaha ya kweli ni kupata kuridhika kwa moyo na roho. Utoshelevu huu wa moyo na roho vinaweza kupatikana tu kwa kutimiza amri za shari’ah na kuimarisha uhusiano wa mtu na Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’alah).

Ikiwa mtu ni mwenye msimamo juu ya Dini na anatekeleza maamrisho ya Shari’ah, basi ingawa yeye hana mengi ya kidunia, atapata furaha na uradhi wa ndani. Kinyume chake, ikiwa mtu hana msimamo katika dini, basi licha ya kumiliki mengi ya ulimwengu, moyo wake utakosa furaha ya kweli.

About admin

Check Also

Kutimiza Amaanah Tunayodaiwa kwa Allah Ta’ala na Viumbe

Katika zama za kabla ya Uislamu na baada ya Uislamu kufika, Uthmaan bin Talhah alikuwa …