Salaam Kwa Nabii ﷺ

Thawabu Maalumu Kwa Ajili Ya Kumsalia Nabii Mara Mia Moja

Sayyidina Abuu Hurairah (radhiyallahu anhu) ameripoti kwamba Nabii wa Allah (sallallahu alaihi wasallam) amesema "yoyote atakaye tuma salaam kwangu mara kumi, Allah subhaana wata'alah atatuma salaam kwake mara mia moja, na yoyote atakaye tuma salaam kwangu mara mia moja, Allah subhaana wata'alah atamtumia salaam kwake mara elfu moja, na yoyote atakaye zidisha (kunisalia mimi) kwa ajili ya upendo (kwa ajili yangu) na kwa hamu (kwa ajili ya kutafuta thawabu), nitamuombea na nitakuwa shahidi kwa ajili yake siku ya mwisho".

Soma Zaidi »

Kupata dua maluum ya wamalaikah

Aamir bin Rabee'ah (radhiyallahu anhu) ameripoti kwamba Nabiii wa allah (sallallahu alaihi wasallam) alisema, "yoyote atakae niswalia, wamalaikah wataendelea kumswalia yeye (yaani: kumuombea dua) kama ataendelea kumswalia Nabii wa allah (sallallahu alaihi wasallam) Kwa hiyo, imebaki kwa mtu kuamua kama atataka kumswalia Nabii wa allah (sallallahu alaihi wasallam) kidogo au kwa wingi."

Soma Zaidi »

Thawabu ya yule ambae anamswalia Nabii wa allah (sallallahu ‘alaihi wasallam) pindi anapo sikia jina tukufu la Nabi wa allah (sallallahu ‘alaihi wasallam)

Anas Bin Maalik (radhiyallahu ‘anhu) ameripoti kwamba Nabii wa allah (sallallahu ‘alaihi wasallam) amesema, "mtu ambae jina langu limetajwa mbele yake anatakiwa atume salamu juu yangu, na kwa hakika yoyote ambae ananitumia salamu mara moja, Allah subhaana wata'alah atamtumia baraka kumi juu yake."

Soma Zaidi »

Kutafuta wema kutoka kwa chanzo chake

Abu hurairah (radhiyallahu anhu) ameripoti kwamba Nabii wa Allah (sallallahu alaihi wasallam) Amesema," yule ambae anasoma quraani tukufu, anamsifu Allah subhaana wata'alah anamswalia Nabii wa Allah (sallallahu alaihi wasallam) Na anaomba msamaha kutoka kwa mola wake basi ametafuta wema kutoka kwa chanzo ya kweli za wema(yaani: amefanya matendo ambayo ni chanzo za wema kwake)."

Soma Zaidi »

Kupata Thawabu Sabini

Abdullah Bin Amr Bin Aas (radhiyallahu ‘anhu) ameripoti, "mtu yoyote atakaye mswalia Nabii wa Allah (sallallahu ‘alaihi wasallam) mara moja, Allah subhaana wata'alah na malaika wake watamtumia rehema na baraka sabini juu yake kwa kumrudishia salaam yake ile ile moja. Baada ya hapo mtu yoyote atakae taka kuzidisha salaam zake azidishe, na yoyote atakae taka kupunguza hapunguze (yaani kama anataka kupata thawabu nyingi, basi azidishe salaam zake).

Soma Zaidi »

Usaidizi Kwenye Daraja La Swirat

عن عبد الرحمن بن سمرة قال: خرج رسول الله صلى الله عليه وسلم فقال: …ورأيت رجلا من أمتي يزحف على الصراط مرة ويجثو مرة ويتعلق مرة فجاءته صلاته علي فأخذت بيده فأقامته على الصراط حتى جاوز… (الأحاديث الطوال للطبراني صـ ٢٧٣، وإسناده ضعيف كما في مجمع الزوائد، الرقم: ١١٧٦٤) Sayyidina …

Soma Zaidi »

Namna Ya Kujisafisha Kutoka Kwenye Madhambi

Abuu Hurairah (radhiyallahu 'anhu) ameripoti kuwa Nabii wa Allah (sallallahu 'alaihi wassallam) amesema, "nisalieni kwa hakika ni njia ya usafishaji wenu. Muulize Allah subhaana wata'alah anijalie daraja la "waswila" ambayo ni daraja la juu la peponi limehifadhiwa kwa mtu mmoja tu, na ninamatumaini yangu kwamba mimi ni yule ambaye amebarikiwa na hii heshima na daraja.

Soma Zaidi »

Kupata Qiraat Moja Ya Thawabu

Sayyidina Ally Bin Abii Taalib (radhiyallahu 'anhu) anaripoti kuwa Nabii (sallallahu 'alaihi wassallam) amesema, "yoyote atakae niswalia mara moja, Allah subhaana wata'alah atamuandikia kirati moja ya thawabu, na kirati moja ni sawa na mlima wa uhudi.

Soma Zaidi »