Usaidizi Kwenye Daraja La Swirat

عن عبد الرحمن بن سمرة قال: خرج رسول الله صلى الله عليه وسلم فقال: …ورأيت رجلا من أمتي يزحف على الصراط مرة ويجثو مرة ويتعلق مرة فجاءته صلاته علي فأخذت بيده فأقامته على الصراط حتى جاوز… (الأحاديث الطوال للطبراني صـ ٢٧٣، وإسناده ضعيف كما في مجمع الزوائد، الرقم: ١١٧٦٤)

Sayyidina Abur Rahmaan Bin Samurah (radhiyallahu ‘anhu) ameripoti: wakati mmoja, Nabii wa Allah (sallallahu ‘alaihi wasallam) alikuja kwetu na akasema, “usiku wa jana, niliona kitu cha ajaabu kwenye ndoto. Nilimuona mtu katika umati wangu alikuwa akivuka daraja la swiraat (daraja lenye lipo juu ya jahannam). Kuna wakati alikuwa akitambaa, wakati mwingine alikuwa akijiburuza kwenye makalio yake, wakati mwingine alikuwa ananing’inia kwenye daraja la swiraat (karibu ya kuanguka ndani ya jahannam). Ghafla, salaam zake alizokuwa ananitumia mimi duniani zimemfikia. Zikaja zikamshika mkononi, zilimsaidia kusimama kwenye daraja la swiraat na zikamsaidia kuvuka juu yake.”

Uzoefu Wa Sheikh Abul Khair Aqtaa (rahimahullah)

Sheikh Abul khair Aqtaa anasema: pindi nilipokuja madina munawwara na nikaishi siku tano pale, nilipitiwa na hali ugumu na njaa. Kwa hiyo nilienda kwenye kaburi ilio barikiwa la Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) nikamsalimia, na nikaenda pia kwenye kaburi la Abu Bakr na Umar (radhiyallahu ‘anhuma) nikamuambia Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam) ewe Nabii wa Allah, (sallallahu ‘alaihi wasallam) leo nataka niwe mgeni wako”. Baada ya hapo, nilitoka kwenye sehemu ile na nikaenda kulala nyuma ya mimbar. Ndotoni, nilimuona Nabii wa Allah (sallallahu ‘alaihi wasallam) pamoja na Abu Bakr (radhiyallahu ‘anhu) upande wake wa kulia, na Umar (radhiyallahu ‘anhu) upande wake wa kushoto na Alli (radhiyallahu ‘anhu) mbele yake. Alli (radhiyallahu ‘anhu) alikuja kwangu na akaniambia, “Inuka, Nabii wa Allah (sallallahu ‘alaihi wasallam) anakuja”. Niliamka kutoka sehemu yangu ya kulala kwa haraka na nikambusu Nabii wa Allah (sallallahu ‘alaihi wasallam) katikati ya macho yake. Alinipa mkate. Mkate huu nilikula nusu yake na nikaacha nusu nyingine. Pindi nilipoamka kwenye ndoto, ile nusu nyingine wa mkate ilikuwa bado ipo mikononi mwangu. (Al- Qawlul Badee’ pg.338)

About admin

Check Also

Chanzo cha nuru siku ya Qiyaama

عن ابن عمر رضي الله عنهما قال قال رسول الله صلى الله عليه وسلم زينوا …