Kupata Radhi Za Allah Subhaana Wata’ Allah

عن عائشة قالت قال رسول الله صلى الله عليه وسلم من سره أن يلقى الله وهو عليه راض فليكثر الصلاة علي (الكامل في ضعفاء الرجال ٦/٣٢، وإسناده ضعيف كما في القول البديع صـ ٢٦٧)

Sayyidatuna Aisha (radhiyallahu ‘anha) ameripoti kwamba Nabii wa Allah (sallallahu alaihi Wasallam) amesema, “yoyote anayetaka kukutana na Allah subhaana wata’alah katika hali Allah subhaana wata’alah yupo radhi naye inabidi anisalie mimi kwa wingi.”

Kisa Cha Ebrahim Bin Khawaas (rahimahullah)

Imeripotiwa kutoka “nuzhatul Basateen” kwamba Ebrahim Bin Khawaas (rahimahullah) amesema wakati mmoja, ndani ya safari, nilikuwa na kiu kikali mpaka ni kaanguka chini na nikazimia. Wakati nilipokuwa nimelala pale, nilihisi mtu ananinyunyizia maji kwenye uso wangu. Pindi nilipofungua macho yangu, nilimuona kijana mzuri juu ya farasi karibu yangu. Alinipa maji ya kunywa na hakanibembeleza niende nae. Baada ya safari kidogo, aliniuliza “unaona nini? Nikajibu, “hii ni madina munawwara. Kisha akasema, “unaweza kusimama hapa. Nenda katika kaburi tukufu la Nabii wa Allah (sallallahu alaihi wasallam) na mfikishie salaamu zangu muambie kwamba kaka yake, khidar, amemfikishia salamu kwake.” (Fazaaile Durood Pg.187)

About admin

Check Also

Chanzo cha nuru siku ya Qiyaama

عن ابن عمر رضي الله عنهما قال قال رسول الله صلى الله عليه وسلم زينوا …