Sunna na Adabu

Dua

Dua ni njia ambayo mja huchota kutoka katika hazina zisizo na mipaka za Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’aala). Kuna fadhila nyingi zilizoripotiwa ndani ya Hadith kwa wale wanao omba dua. Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam) amesema kwamba dua ni asili ya ibaadah zote.[1]  Katika Hadith nyingine, Mtume (Sallallahu ‘alaihi wasallam) ametaja kuwa …

Soma Zaidi »

Sura Maalum Kwenye Nyakati na Matukio Mbalimbali 5

10. Soma Sura Fatiha na Sura Ikhlaas kabla ya kulala. Anas (radhiyallahu ‘anhu) anasema kwamba Mtume (Sallallahu ‘alaihi wasallam) alisema, “(Wakati wa kulala,) unapoweka ubavu wako juu ya kitanda, na ukasoma Sura Faatihah na Sura Ikhlaas, basi utasalimika na kila kitu isipokuwa kifo.”[1] 11. Soma Surah Zumar na Surah Bani …

Soma Zaidi »

Sura Maalum Kwenye Nyakati na Matukio Mbalimbali 4

8. Soma Surah Kahf siku ya Ijuma. Ibnu Umar (radhiyallahu anhuma) anasimulia kwamba Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam) amesema: “Mwenye kusoma Surah Kahf siku ya ijuma, nuru (mwanga) hutoka chini ya miguu yake na kupanuka hadi kufika angani. Nuru hii itan’gaa siku ya Qiyaamah, na madhambi yake yote (madogo) atakayofanya katikati …

Soma Zaidi »

Sura Maalum Kwenye Nyakati na Matukio Mbalimbali 3

6. Soma Surah Sajdah kabla ya kulala. Jaabir (radhiyallahu ‘anhu) anaripoti kwamba Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam) alikuwa halali mpaka asome Surah Sajdah na Surah Mulk.[1] Khaalid bin Ma’daan (rahimahullah), ambae ni Taabi‘i, ametaja yafuatayo:“Hakika Sura Sajdah itabishana kaburini kwa kumtetea mwenye kuisoma. Itasema, ‘Ewe Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’aala)! Ikiwa nipo …

Soma Zaidi »

Qunoot

4. Jinsi ya kutekeleza rakaa tatu za Witr ni kwamba utaswali rakaa mbili kwanza na kutoa salaam. Baada ya hapo utaswali rakaa moja. Ukipenda unaweza kuswali rakaa mbili na kukaa kwa ajili ya tashahhud. Kisha utasimama na kutekeleza rakaa ya tatu. Katika hali zote mbili, Qunuut itasomwa katika rakaa ya …

Soma Zaidi »

Qunoot

3. Ni sunna kuswali Witr kila siku katika kipindi chote cha mwaka. Swala ya Witr itatekelezwa baada ya kuswali Fardh na Sunnah za Swalah ya Esha. Kwa mwaka mzima, mtu anaposwali Witr, hatosoma Qunoot. Lakini, ni sunna kusoma Qunout kwenye Witr katika kipindi cha pili ya Ramadhaan (tangu 15 Ramadhani …

Soma Zaidi »

Sura Maalum Kwenye Nyakati na Matukio Mbalimbali 2

4. Soma Surah Yaseen kila asubuhi na jioni. Ibnu Abbaas (radhiyallahu anhuma) anaripoti kwamba, “Yoyote anayesoma Sura Yaaseen asubuhi, kazi yake ya siku hiyo nzima itarahisishwa, na yoyote atakayeisoma mwisho wa siku, kazi yake mpaka asubuhi itarahisishwa.”[1] Jundub (radhiyallahu anhu) anasimulia kwamba Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam) amesema: “Mwenye kusoma Sura …

Soma Zaidi »

Qunoot

1. Ni Sunnah kusoma Qunoot katika rakaa ya pili ya Alfajiri. Qunoot itasomwa katika rakaa ya pili pindi unaposimama baada ya rukuu. Mtu atasoma kwanza tahmiid (ربنا لك الحمد) na baada ya hapo ataisoma Qunout. 2. Wakati wa kusoma Qunoot, mtu atainua mikono yake sambamba na kifua chake na kufanya …

Soma Zaidi »

Sura Maalum Kwenye Nyakati na Matukio Mbalimbali 1

Kuna baadhi ya surah ambazo zinatakiwa kusomwa kwenye nyakati maalum wakati wa usiku na mchana au katika siku fulani ndani ya week. Ni mustahab kwa mtu kusoma surah hizi kwa muda wake. 1. Soma Surah Kaafirun kabla ya kulala Imepokewa kutoka kwa Jabalah bin Haarithah (radhiyallahu ‘anhu) kwamba Mtume (Sallallahu …

Soma Zaidi »

Qa’dah Na Salaam

7. Ikiwa ni qa’dah ya mwisho, basi soma tashahhud, Swalawaat Ebrahimiyyah na baada ya hapo fanya dua. Swalawaat Ibrahimiyyah ni ifuatavyo: اَللّٰهُمَّ صَلِّ عَلٰى مُحَمَّدٍ وَّعَلٰى اٰلِ مُحَمَّدٍ كَمَا صَلَّيْتَ عَلٰى إِبْرَاهِيْمَ وَعَلٰى اٰلِ إِبْرَاهِيْمَ  وَبَارِكْ عَلٰى مُحَمَّدٍ وَّعَلٰى اٰلِ مُحَمَّدٍ كَمَا بَارَكْتَ عَلٰى إِبْرَاهِيْمَ وَعَلٰى اٰلِ إِبْرَاهِيْمَ فِيْ الْعَالَمِيْنَ …

Soma Zaidi »