Sunnat Na Adabu Za Kuamkiana (Kutoa Salaam) 2

4. Unatakiwa kutoa salaam kwa kusema “Assalaamu alaikum” unaweza pia kutoa salaam kwa kusema “Assalaamu alaikum wa rahmatullah” au “Assalaamu alaikum wa rahmatullahi wa barakaatuhu”. Kwa kutoa salaam ndefu, utapata thawabu zaidi.

Imraan bin Husein (radhiyallahu anhu) anasimulia kwamba mtu mmoja alikuja kwa Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) na akamsalimia akisema: “Assalaamu alaikum.” Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) akajibu salaam yake kisha huyo mtu akakaa kwenye mkusanyiko. Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) akasema: “Amepata thawabu kumi.” Baadaye, mtu mwingine alikuja kwa. Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) na akamsalimia akisema: “Assalaamu alaikum wa rahmatullah.” Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) akajibu salamu na mtu huyo akaketi kwenye mkusanyiko. Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) akasema, “Amepata thawabu ishirini.” Baada ya hapo, mtu mwingine alikuja kwa Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) na akamsalimia akisema: “Assalaamu alaikum wa rahmatullahi wa barakaatuh.” Mtume (sallallahu alaihi wasallam) akamjibu na mtu huyo akakaa pia kwenye mkusanyiko. Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) akasema: “Amepata thawabu thalathini.”[1]

5. Mwislamu akikusalimu kwa salaam, itakuwa ni lazima wewe kujibu salamu, isipokuwa kama una udhuru ya halali k.m. unakula, unasoma Quran Majeed n.k. Ingawa si lazima kwako kujibu salamu katika hali hizi, inajuzu kwako kujibu.

6. Ni makrooh kumsalimia mtu anayehusika na shughuli yoyote ya Deeni au akiwa anakula n.k.

7. Usitoe salaam kwa wasio maharimu (watu ambao unaweza kuwaowa). Ikiwa mwanamke Mahram akamsalimia mwanamume, basi akiwa ni mzee ambaye hakuna khofu ya fitna juu yake, basi mtu anaweza kumjibu salamu. Lakini, ikiwa ni mschana anayetoa salamu, basi mtu hatakiwi kujibu salamu kwa maneno. Bali mtu anaweza kujibu salamu ndani ya moyo wake.

AUD-20240911-WA0000


[1] سنن أبي داود، الرقم: 5197، سنن الترمذي، الرقم: 2689 وقال الترمذي: هذا حديث حسن غريب من هذا الوجه

About admin

Check Also

Salaam

Salaam ni kumsalimia muislamu. Kama vile Uislamu unavyosimamia amani, maamkizi ya Uislamu ni salamu ya …