4. Unapowatembelea wagonjwa, soma dua ifuatayo:
لَا بَأْسَ طَهُوْرٌ إِنْ شَاءَ اللهُ
Hakuna haja ya kuwa na wasiwasi, kupitia maradhi haya, utatakasika inshaAllah.[1]
Unaweza pia kusoma dua ifuatayo mara saba:
أَسْألُ اللهَ الْعَظِيْمَ رَبَّ الْعَرْشِ الْعَظِيْمِ أَنْ يَّشْفِيَكَ
Ninamuomba Allah Ta’ala, Mola wa Arshi kubwa, akuponye.
Imepokewa kutoka kwa Ibnu Abbaas (radhiyallahu ‘anhuma) kwamba Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam) alisema mtu anayesomea mgonjwa dua hiyo mara saba ambaye hakukusudiwa kufa katika ugonjwa huo, basi Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’aala) atamponya na ugonjwa huo.[2]
5. Ikiwa haitaleta usumbufu wowote kwa mgonjwa, basi unaweza kumuomba mgonjwa akuombee dua kwa Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’aala) kwa niaba yako.
Umar (radhiyallahu ‘anhu) anaripoti kwamba Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam) alisema, “wakati alipomtembelea mgonjwa, (ikiwezekana kumuomba akuombee dua) basi muombe akuombee dua, kwa hakika dua yake ni sawa sawa na dua ya Malaika (kwa sababu madhambi yake yamesafishwa).”[3]
6. Sunnah ya kumtembelea mgonjwa haipo tu kwa wanafamilia au marafiki. Iwapo mtu anamjua Muislamu yoyote ambaye ni mgonjwa, na ikawezekana kwenda kumzuru, basi afanye hivyo.
Kumbuka: Imepokewa kwamba Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam) alimtembelea mtoto wa kiyahudi aliyekuwa mgonjwa, na Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) akaampa da’wa ndani ya Uislamu. Mtoto huyo alisilimu na kisha akafariki.
Kwa hivyo, Maulamaa wanaeleza kwamba kafiri akiugua, basi inajuzu kumtembelea. Wakati wa kumtembelea, mtu afanye nia ya kuumpa da’wa ndani ya Uislamu.
Inapaswa iyeleweke kwamba kumtembelea kafiri itakuwa inajuzu tu kwa sharti kwamba mtu ana yakini kwamba hatoharibu Dini yake kwa njia yoyote ile. Kwa hivyo, ikiwa kuna kitu kinyume na Uislamu (k.m. kuna msalaba ndani ya nyumba, kuna muziki inachezwa, kuchanganywa kwa wanaume na wanawake, picha au sanamu, nk) basi katika matukio haya yote, haitajuzu kwa mtu kumtembelea kafiri.
[1] صحيح البخاري، الرقم: 5656
[2] سنن أبي داود، الرقم: 3106، سنن الترمذي، الرقم: 2083، وقال: هذا حديث حسن غريب لا نعرفه إلا من حديث المنهال بن عمرو
[3] سنن ابن ماجة، الرقم: 1441، وإسناده حسن كما في مسند الفاروق لابن كثير 1/228