Kupokea Cheo Cha ‘Msaidizi Maalum’ wa Mtume (Sallallahu ‘alaihi wasallam)

Katika tukio la Vita vya Ahzaab, vilivyojulikana pia kama Vita vya Khandaq, Waislamu walipata habari kwamba Banu Quraidhah wamevunja kiapo chao cha kumtii Mtume (Sallallahu ‘alaihi wasallam) na wamejiunga na maadui. Ili kuhakikisha taarifa hizo, Mtume (Sallallahu ‘alaihi wasallam) aliwauliza Maswahabah (Radhiya Allaahu ‘anhum), “Ni nani atakayeniletea habari za watu hawa (Banu Quraidhah)?” Zubair (Radhiya Allaahu ‘anhu) alijibu mara moja kwa kujitolea kwenda kama jasusi na kuleta taarifa za Banu Quraidhah kwa Mtume (Sallallahu ‘alaihi wasallam).

Baada ya muda, Mtume (Sallallahu ‘alaihi wasallam) akauliza tena: “Ni nani atakayeniletea habari za watu hawa (Banu Quraidhah)?” Kwa mara nyingine tena, Zubair (Radhiya Allaahu ‘anhu) alijitolea kwenda. Hatimaye, Mtume (Sallallahu ‘alaihi wasallam) akauliza kwa mara ya tatu, “Ni nani atakayeniletea habari za watu hawa (Banu Quraidhah)?” Mara hii pia, Zubair (Radhiyallahu ‘anhu) alijitolea kwenda. Ilikuwa ni katika tukio hili ambapo Mtume (Sallallahu ‘alaihi wasallam) alifurahishwa na Zubair (Radhiya Allaahu ‘anhu) na akataja, “Hakika kila Nabii alikuwa na msaidizi maalum, na msaidizi wangu maalum ni Zubair bin ‘Awwaam (Radhiya Allaahu ‘anhu).” (Siyar A’laam min Nubalaa 3/30, Sahih Bukhaari #3719, Sahih Muslim #2415, Sunan Tirmidhi #3745, Fat-hul Baari 6/63, 7/100)

About admin

Check Also

Ukarimu Na Zuhd (Kujiepusha na dunia) Wa Abu Ubaidah (Radhiya Allaahu ‘anhu)

Wakati mmoja, Umar (Radhiya Allaahu ‘anhu) alichukua sarafu za dhahabu mia nne, akaziweka kwenye mfuko …