Sunnah na Adabu Za Kuwatembelea Wagonjwa 1

1. Ni mustahabu kufanya wudhu kabla ya kumtembelea mgonjwa.[1]

Anas (radhiyallahu ‘anhu) anasema kwamba Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam) alisema, “Mwenye kufanya wudhu kamili (yaani kwa kutimiza sunnah na vitendo vya mustahab vya wudhu) na akafunga safari kwenda kumtembelea ndugu yake Mwislamu mgonjwa kwa matumaini ya kupata thawabu za kumtembelea mgonjwa, mtu huyo atawekwa mbali na moto wa Jahannamu kwa urefu wa miaka sabini.”[2]

2. Unapomtembelea mgonjwa, uskaai muda mrefu, na hivyo kumsababishia mgonjwa usumbufu. Badala yake, unapaswa kuondoka baada ya muda mfupi.

Imepokewa kwamba Ibnu Abbaas (radhiyallahu ‘anhu) amesema, “ni katika Sunnah kufupisha ziara ya mtu (mgonjwa) na kuepuka kupiga kelele.”[3]

3. Kuwafariji wagonjwa na kumpa moyo na matumaini kupona. Sio sahihi kwa daktari au mtu yoyote kumjulisha mgonjwa kwamba hakuna tumaini lililobaki kwake katika hali yoyote.

Imepokewa kutoka kwa Abu Sa’id Khudri (radhiyallahu ‘anhu) kwamba Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) alisema: “Unapomtembelea mgonjwa, basi mpe faraja na matumaini ya maisha, kwa kumpa matumaini (na kuinua roho yake) haitabadili taqdeer. Lakini, itakuwa njia ya kumletea furaha na faraja.”[4]

Ibnu Abbaas (radhiyallahu ‘anhu) anaripoti kwamba Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam) wakati mmoja alimtembelea mwanakijiji mgonjwa, na kila alipokuwa akiwatembelea wagonjwa, alikuwa akisoma dua ifuatayo:

لَا بَأْسَ طَهُوْرٌ إِنْ شَاءَ اللهُ

Hakuna haja ya kuwa na wasiwasi, kupitia maradhi haya, utatakasika na inshaAllah.[5]

AUD-20240529-WA0000


[1] من عاد متوضيًا ويكون فائدة الوضوء أنه ربما يطلب المريض الدعاء منه فيدعو له، وعلى الثاني فينبغي أن يكون الوضوء مستحبًا للعيادة (فتح الودود في شرح سنن أبي داود 3/ 384)

(عن أنس بن مالك قال: قال رسول الله – صلى الله عليه وسلم -: من توضأ فأحسن الوضوء) أي: أسبغه (4) وأتمه، أو أتى بآدابه وسننه، وفيه استحباب العيادة على وضوء شرح سنن أبي داود لابن رسلان 13/ 288)

[2] سنن أبي داود، الرقم: 3097، سكت عنه الحافظ في الفصل الثاني من هداية الرواة (2/163) وقد قال في مقدمته (1/58): وما سكت عن بيانه فهو حسن

[3] مرقاة المفاتيح 3/1153

[4] سنن الترمذي، الرقم: 2087، وقال هذا حديث غريب

[5] صحيح البخاري، الرقم: 5656

About admin

Check Also

Fadhila Za Kutoa Salaam

Fadhila Ya Kutoa Salaam Wakwanza Abdullah bin Mas’uud (Radhiya Allaahu ‘anhu) anasimulia kwamba Mtume (Sallallahu …