Kutimiza Amaanah Tunayodaiwa kwa Allah Ta’ala na Viumbe

Katika zama za kabla ya Uislamu na baada ya Uislamu kufika, Uthmaan bin Talhah alikuwa mlinzi wa ufunguo wa Ka’ba. Alikuwa akifungua Ka’bah siku za jumatatu na alhamisi, akiwaruhusu watu kuingia na kujishughulisha na ibaadah.

Wakati mmoja, kabla ya hijrah, watu walipokuwa wakiingia ndani ya Ka’bah katika hizo siku, Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) pia alitaka kuingia. Lakini, Uthmaan bin Talhah hakumruhusu kuingia na akamwambia maneno za jeuri na ukali.

Mtume (Sallallahu ‘alaihi wasallam) alivumilia maneno yake makali na akamwambia: “Ewe Uthmaan! Siku inakuja ambapo utaona funguo za Ka’ba mkononi mwangu, na nitakuwa na uwezo wa kumpa nimtakaye.”

Uthmaan akajibu akisema: “Siku hiyo itakuwa ni siku ya kudhalilishwa kwa Maquraishi! Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam) akasema, “Hapana! Bali itakuwa siku yenye heshima kubwa kwa Maquraishi.”

Uthmaan bin Talhah anasema, “Nilijua kwamba siku hio hakika itakuja na nilikuwa na yakini kamili kwamba yale aliyoyasema Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam) yatatokea.

Kwa hio, wakati ulifika ambapo Allah Ta’ala alimwamrisha Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam) na Maswahabah (radhiyallahu anhum) kuhijiria Madinah Munawwarah, na vita vingi vikali vikafuatana baina ya Waislamu na Maquraishi katika miaka iliyofuata.

Kisha ukaja wakati ambapo Allah Ta’ala akaujalia moyo wa Uthmaan bin Talhah kusilimu. Kwa hiyo, aliondoka Makka Mukarramah kwenda Madina Munawwarah katika mwaka wa 7 baada ya hijrah kusilimu na kuweka kiapo cha utii mikononi wa Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam)

Mwaka mmoja baadaye, katika tukio la Fath-ul-Makkah, Mtume (Sallallahu ‘alaihi wasallam) alimuagiza Uthmaan bin Talhah (radhiyallahu ‘anhu) kumletea funguo za Ka’bah, kwa vile funguo zilikuwa chini ya uangalizi wa familia yake.

Baada ya kuleta funguo, Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) aliingia ndani ya Ka’bah na kufanya ibaadah. Baada ya hapo, Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam) alipotoka ndani ya Ka’bah, Abbaas na Hazrat Ali (radhiyallahu ‘anhuma) wote walitaka kupewa heshima ya kuwa wasimamizi wa funguo za Ka’bah.

Wakati Mtume (Sallallahu ‘alaihi wasallam) alikuwa ndani ya Ka’bah, Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’aala) aliteremsha aya ifuatayo ya Qur’an, akimwagiza kurudisha amana Uthmaan bin Talha (radhiyallahu ‘anhu) na familia yake.

Allah Ta’ala alisema:

إِنَّ اللَّهَ يَأْمُرُكُمْ أَن تُؤَدُّوا الْأَمَانَاتِ إِلَىٰ أَهْلِهَا

Hakika Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’aala) anakuamrisheni mrejeshe amana kwa waliostahiki.

Kisha Mtume (Sallallahu ‘alaihi wasallam) akarudisha funguo kwa Uthmaan bin Talhah (radhiyallahu ‘anhu), na akamwambia kwamba funguo zitabaki na familia yake, na kwamba hakuna yoyote atakayezichukua kutoka kwao isipokuwa dhalimu.

Wakati Uthmaan bin Talhah (radhiyallahu ‘anhu) alipokuwa anaondoka na funguo, Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) alimwita na kusema, “Ewe Uthmaan! Je, unakumbuka niliyokuambia hapo awali, kwamba siku inakuja ambapo utaona funguo za Ka’ba mkononi mwangu, na nitakuwa na uwezo wa kumpa yoyote nimtakaye?”

Uthmaan bin Talhah (radhiyallahu ‘anhu) akajibu, “Ndiyo, Ewe Rasulullah! Nakumbuka siku hiyo!”

Kutokana na aya iliyotajwa hapo juu ya Quraan Takatifu, tunajifunza kwamba amana zote zinapaswa kurejeshwa kwa wale wanaostahiki kuzipata. Ndani ya mahadith, Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) ameweka msisitizo mkubwa katika kutimiza amana.

Kila Mtu Anajukumu la Kutimiza Uaminifu Wake

Inapaswa kueleweka kuwa kutimiza amana sio tu mali ambayo imekabidhiwa kwa mtu, lakini inajumuisha kila aina la jukumu (iwe ya kidunia au lq deeni) ambayo mtu kapewa.

Imamu wa msikiti, muadhini, mutawalli (mdhamini wa shirika la msikiti au deeni), mtawala au watu chini yake, mwalimu au mwanafunzi, mwajiri au mfanyakazi, mnunuzi au muuzaji, mume au mke, wazazi au watoto, majirani au washirika – wote wamekabidhiwa amana wanao daiwa na Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’alah) na kwa viumbe. Kwa hivyo, amana kubwa zaidi, ambayo itajumuisha amana zote, ni amana ya Dini.

Allah Ta’ala atujaalie tawfeeq ya kutimiza amana hii kwa usahihi, kwa mujibu wa hukm za shari’ah.

About admin

Check Also

Swalaah – Ufunguo wa Jannah

Uislamu ndio njia pekee inayoongoza kwenye mapenzi ya Allah Ta’ala na inaongoza kwenye Jannah. Kupitia …