Abdullah bin Zubair (Radhiya Allaahu ‘anhu) anasimulia kwamba wakati fulani alimuuliza baba yake, Zubair (Radhiya Allaahu ‘anhu), “Kwa nini usimuli mahadith za Mtume (Sallallahu ‘alaihi wasallam), kama vile maswahaabah (Radhiya Allaahu ‘anhum) wengine?”
Zubair (Radhiya Allaahu ‘anhu) akajibu, “Sikuacha upande wa Rasulullah (Sallallahu ‘alaihi wasallam) baada ya kusilimu (yaani nina uwezo wa kusimulia mahadith nyingi kutoka kwake). Lakini, katika tukio moja, nilimsikia Mtume (Sallallahu ‘alaihi wasallam) akitaja kitu (ambacho nahofia kusimulia mahadith). Nilimsikia Mtume (Sallallahu ‘alaihi wasallam) akisema: “Mwenye kutunga uwongo (anatunga hadith na kuninasibisha) basi ataarishe makazi yake Motoni.” (Siyar A’laam min Nubalaa 3/27)