Dua Za Kusomwa Wakati Wa Kumtembelea Mgonjwa

Dua Ya Kwanza

لَا بَأْسَ طَهُوْرٌ إِنْ شَاءَ اللهُ

Hakuna haja ya kuwa na wasiwasi, kupitia maradhi haya, utatakasika inshaAllah (yaani, hakuna haja ya wewe kuwa na wasiwasi au hofu yoyote. Unapitia mchakato wa utakaso tu. Kiroho, unasafishwa na dhambi zako, na kiafya, mwili wako unasafishwa na sumu. Kwa hivyo, ugonjwa huu unapokujia kama rehema iliyojificha kutoka kwa Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’aala), hakuna haja ya kuwa na wasiwasi na kuhuzunika).[1]

Dua Ya Pili

Soma dua ifuatayo mara saba:

أَسْألُ اللهَ الْعَظِيْمَ رَبَّ الْعَرْشِ الْعَظِيْمِ أَنْ يَّشْفِيَكَ

Namuomba Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’aala), Mola wa Arshi kubwa akupe shifaa.

Imepokewa kutoka kwa Ibnu Abbaas (radhiyallahu ‘anhuma) kwamba Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam) amesema: “Yoyote atakayesoma dua ifuatayo mara saba kwa mgonjwa ambaye hakujaaliwa kufa katika ugonjwa huo, Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’aala) atamponya na ugonjwa huo:

أَسْألُ اللهَ الْعَظِيْمَ رَبَّ الْعَرْشِ الْعَظِيْمِ أَنْ يَّشْفِيَكَ[2]

Dua ya Tatu:

أَذْهِبِ الْبَأْسَ رَبَّ النَّاسِ وَاشْفِ أَنْتَ الشَّافِيْ لَا شِفَاءَ إِلَّا شِفَاؤُكَ شِفَاءً لَا يُغَادِرُ سَقَمًا

Ondoa matatizo, ewe Mola wa watu wote, na umpe tiba – Wewe Peke Yako ndio unao uwezo wakuponya, hakuna tiba ila tiba yako- (umpe) tiba ambayo haitaacha ugonjwa.[3]

Dua Ya Nne:

بِاسْمِ اللهِ أَرْقِيْكَ مِنْ كُلِّ شَيْءٍ يُؤْذِيْكَ مِنْ شَرِّ كُلِّ نَفْسٍ أَوْ عَيْنٍ حَاسِدٍ اللهُ يَشْفِيْكَ بِاسْمِ اللهِ أَرْقِيْكَ

Kwa jina la Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’aala) Ninakusomea (kutafuta tiba kutoka kwa Allah Ta’ala) kutokana na kila jambo linalokudhuru- kutoka kwa kila nafsi (mbaya) au jicho lenye husda. Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’aala) akupa tiba. Kwa jina la Allah Ta’ala nakusomea.[4]


[1] صحيح البخاري، الرقم: 5656

[2] سنن أبي داود، الرقم: 3106، سنن الترمذي، الرقم: 2083، وقال: هذا حديث حسن غريب لا نعرفه إلا من حديث المنهال بن عمرو

[3] صحيح البخاري، الرقم: 5750

[4] صحيح مسلم، الرقم: 2186

About admin

Check Also

Sunnah Na Adabu Za Kuwatembelea Marehemu 4

14. Wasaidie waliofiwa kwa kuwapelekea chakula nyumbani kwao. Mtume (Sallallahu ‘alaihi wasallam) amewafundisha Maswahaba (radhiyallahu …