Kuwafariji Wafiwa

Uislamu ni mfumo mpana na mkamilifu zaidi wa maisha ambao umezingatia kila hitaji la mwanadamu. Haikuonyesha tu njia ya amani kwenye maisha ya mtu, lakini pia imeonyesha jinsi ya kuonyesha upendo na amani baada ya kifo cha mtu. Hivyo basi, Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam) kupitia mafundisho yake matukufu na kwa mfano wake uliobarikiwa, alionyesha Ummah jinsi ya kuwafariji wafiwa walio na msiba.

Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam) amesema: “Mwenye kumfariji mtu aliye na shida atapata thawabu sawa na yule aliyefiwa (yaani malipo anayopata mfiwa kwa kuvuta subra katika shida yake).

Katika Hadiyth nyingine, Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam) amesema, “Hakuna
muumini ambaye humfariji ndugu yake Mwislamu wakati wa matatizo isipokuwa kwamba Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’alah) atamvisha nguo za heshima Siku ya Qiyaamah.”

Sunnah Na Adabu Za Kuwatembelea Marehemu

1. Ta’zia maana yake ni kumpa pole mfiwa na kuwahurumia walio ondokewa na wapendwa wa karibu. Hili litafanyika kwa kumuombea dua marehemu mbele ya familia. Vile vile, hili litafanywa kwa kuomba dua kwa ajili ya familia, kumuomba Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’alah) awabariki na uvumilivu katika mtihani huu.

2. Mtu anaweza kuomba dua kwa maneno yafuatayo, “Allah Ta’ala ampe marehemu hatua za juu kabisa katika Jannah na msamehe madhambi yake,” na “Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’alah) aijaalie familia sabr-un-jameel (uvumilivu mzuri).”

AUD-20240717-WA0005

About admin