Ukarimu Wa Zubair (Radhiya Allaahu ‘anhu)

Hishaam bin ‘Urwah anataja kwamba maswahaabah saba (Radhiya Allaahu ‘anhum) walimchagua Zubair (Radhiya Allaahu ‘anhu) kuwa mtekelezaji wa mali zao baada ya kufariki kwao. Miongoni mwa hawa maswahaabah (Radhiya Allaahu ‘anhum) walikuwa ‘Uthmaan (Radhiya Allaahu ‘anhu), ‘Abdur Rahmaan bin ‘Auf (Radhiya Allaahu ‘anhu), Miqdaad (Radhiyallahu ‘anhu) na ‘Abdullah bin Mas’uud (Radhiyallahu ‘anhu). Baada ya kufariki kwao, Zubair (Radhiya Allaahu ‘anhu) alihifadhi mali zao kwa ajili ya watoto wao wadogo na alikuwa akitumia mali yake binafsi kwenye mahitaji yao. (Usdul Ghabah 2/211)

About admin

Check Also

Uhuru wa Bilaal (Radhiyallahu ‘Anhu) na hamu ya Rasulullah (Sallallahu’ Alaihi Wasallam) kwa Bilaal (Radhiyallahu ‘Anhu) kuwa huru

Wakati mmoja, wakati akizungumza kuhusu Bilaal (Radhiyallahu 'Anhu), Sa'eed bin Musayyib (Rahimahullah) alisema:

Tamaa ya kuwa muisilamu ilikuwa kubwa sana moyoni mwa Bilal (Radi Allahu 'Anhu). Alikuwa akiwekwa chini na kuteswa katika mikono ya makafiri. Wakati wowote makafiri wangejaribu kumlazimisha kuachana na Uislamu, angekataa kwa nguvu na kutangaza waziwazi "Allah Allah" (yaani Allah Ta'ala ndiye mungu pekee anayestahili kuabudiwa).

Rasulullah (Sallallahu 'Alaihi Wasallam) kisha alikutana na Abu Bakr (Radhiyallahu' Anhu) na alionyesha hamu yake akisema, "Ikiwa tu tungekuwa na mali ambayo tunaweza kumnunua Bilaal (na kumwachisha huru)!" Baada ya hapo, Abu Bakr (Radhiyallahu 'Anhu) alimkaribia 'Abbaas (Radhiyallahu' Anhu) akamwambia, "Nenda umnunue Bilaal kwa niaba yangu."