Abul Aswad anasimulia yafuatayo: Zubair (Radhiya Allaahu ‘anhu) alisilimu na umri wa miaka minane, na akafanya hijrah akiwa na umri wa miaka kumi na nane. Mjomba wake alikuwa akimweka ndani la kibanda kidogo na kuwasha moto ili ateseke na moshi huo. Kisha mjomba wake angemuamuru kuu achana Uislamu, ambao alikuwa akijibu, “Sintokuwa kafiri kamwe”
Zubair (Radhiya Allaahu ‘anhu) alikuwa miongoni mwa Maswahaabah (Radhiya Allaahu ‘anhum) waliofanya Hijrah hadi Abyssinia ili kuepuka na mateso ya Maquraishi. Hata hivyo, hakukaa muda mrefu huko Abyssinia, mpaka aliporejea Makka Mukarramah na kisha akahijiria kwenda Madina Munawwarah. Hivyo, alibarikiwa kwa heshima ya kushiriki katika hijra zote mbili kwa ajili ya Uislamu (Tahdheeb-ul-Kamaal 9/321, Siyar A’laam min Nubalaa 3/30)
Audio Player