Sifa Ya Amaanah – Fikra Ya Kuulizwa

Allah Ta’ala amemneemesha mwanadamu kwa neema zisizohesabika. Baadhi ni neema za kimwili, wakati nyingine ni neema za kiroho.

Mara nyingi, kuna neema nyingi ambazo zinahusishwa na neema mmoja. Fikiria neema ya macho – ni njia ya mtu kuona maelfu ya neema zingine za Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’alah). Hata hivyo, kuona ni miongoni za neema za kimwili za Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’alah).

Miongoni mwa neema za kiroho za Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’alah) ni sifa ya amaanah (fikra ya kuulizwa). Sifa ya amaanah unazingatiwa miongoni mwa sifa muhimu za Imaan, na umuhimu wake umesisitizwa sana katika Hadith.

Anas (Radhiyallahu ‘anhu) anasimulia kwamba: “Ni mara chache sana Mtume (Sallallahu ‘alaihi wasallam) akitoa khutba na wala asitilie mkazo umuhimu wa Amaanah akisema, ‘Yule ambaye hana Amaana basi hana Imaan kamili, na asiyetimiza ahadi zake hana Dini kamili.”

Amaanah Inahusu Nini?

Sifa ya amaanah inahusu mtu mwenye kuwa na wasiwasi kulizwa katika mahakama ya Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’alah) kuhusiana na faradhi anazodaiwa na Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’alah) na waja wa Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’alah).

Hii ni sifa nzuri sana kwamba ni mlango wa kupata neema zisizohesabika za Allah Ta’ala za kiroho na kimwili. Sifa ya amaanah huunda uhai katika moyo wa kiroho na kuujaza macho ya kiroho.

Kwa hivyo, mtu anapokuwa na sifa ya amaanah, basi moyo wake una uwezo wa kuona jema kama jema na baya kama uovu. Ina uweza wa kutofautisha kati ya yale yenye manufaa kwa mtu na yale yenye madhara kwake.

Kimsingi, amaanah unamshawishi mtu katika uchamungu na uadilifu katika nyanja zote za maisha yake.

Amaanah – Mwonekano wa Kiroho wa Moyo

Kama jinsi mtu anavyohitaji macho ya kimwili ili aweze kufaidika na mwanga wa jua, hivyo ndivyo mtu anavyohitaji macho ya kiroho (yaani sifa wa amaanah) kwa mpangilio ili afaidike na nuru ya Dini (yaani Quran na Sunnah).

Ikiwa mtu hana macho ya kimwili, basi licha ya ulimwengu kuangaza karibu naye, hatoweza kufaidika na uzuri wa ulimwengu.

Vile vile ikiwa mtu hana nuru ya moyo (yaani. amepungukiwa na sifa wa amaanah), basi licha ya kupatikana kwa Qur’aan na Sunnah (ambayo ndiyo ufunguo wa kufaulu katika kumulika maisha ya Muumini kwa furaha), mtu wa aina hiyo hatoweza kufaidika kikamilifu na nuru ya Dini.

Utabiri Wa Mtume (sallallahu alaihi wasallam)

Huzaifah (Radhiyallahu anhu) anasema, “Mtume (sallallahu alaihiwasallam) alitutajia hadith mbili; Nimeshuhudia ya kwanza kutokea, na mimi bado nasubiri kushuhudia ya pili.

“Mtume (Sallallahu ‘alaihi wasallam) ametufahamisha kwamba amaanah uliteremshwa na Allah Ta’ala katika nyoyo za watu. Baada ya hapo, kupitia nuru ya amaanah, watu waliielewa Qur’aan na Sunnah kwa usahihi.

“Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) akatuambia kwamba wakati utafika ambapo amaanah hii itanyanyuliwa taratibu kutoka nyoyo za watu.

“Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) amesema: ‘Mtu atalala na kuamka, na sehemu ya Amaana kutoka moyoni mwake (yaani kwa sababu ya kufanya madhambi, sehemu ya amaanah itaondolewa kutoka moyoni mwake na kusababisha yeye kutokuelewa Dini kwa usahihi na baada ya hapo kuwa mzembe katika kutimiza haki za Allah Ta’ala na waja zake).

“Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) akasema: ‘Watu wataamka asubuhi wakishughulika wao kwa wao, na wala hawatasimamisha Amaana. Wakati huo itasemwa, ‘Katika kabila fulani na fulani, kuna mtu ambaye ana sifa ya amaanah’, na itasemwa kuhusu mtu fulani, ‘Ana akili kiasi gani! Ana busara kama nini! Ana uwezo gani!’, lakini moyo wa mtu kama huyo hautakuwa na hata punje ya Imaan.”

Amaanah Haijawekwa Mipaka kwenye Kulinda Mali Za Watu

Kwa ujumla, inapotajwa sifa ya amaanah, basi akili za watu huenda kwenye kulinda mali ambayo mtu amekabidhiwa.

Hata hivyo, ikumbukwe kwamba sifa ya amaanah haijawekwa mipaka kwa kulinda mali ya mtu yoyote ambaye amemchagua kuwa mdhamini wake.

Bali sifa ya amaanah ni kwamba inajumuika katika kila kitu kwenye maisha ya mtu, iwe ni kuhusiana na faradhi anazodaiwa na Allah Ta‘ala au waja wa AllahTa’ala.

Kwa hivyo, katika maisha ya mtu binafsi, maisha ya kijamii, maisha ya kiuchumi na katika kila nyanja zinginey za deeni ya mtu na maisha ya dunia, mtu anapaswa ajihesabu kuwa ni mwenye ataulizwa katika mahakama ya Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’aala) kuhusu haki anazodaiwa naAllah Ta’ala na waja wake.

Katika nyakati za leo, ikiwa kila mtu atashikilia na sifa ya amaanah katika maisha yake, ndipo amani na maelewano vitatawala duniani. Hakutakuwa na sababu ya mabishano na ugomvi kutokea kati ya ndugu, jamaa, waume na wake, waajiri na wafanyakazi, marafiki, majirani, washirika wa kibiashara, watu wenye mamlaka kama vile wadhamini na walimu, au watu wanaotoa huduma kwa umma kama vile madaktari, wajenzi, mawakili n.k.

Vile vile, wakati wa kusambaza mali ya aliyefariki, hakuna mtu atakayedhulumiwa wala haki ya mtu yoyote itachukuliwa, kwani kila mtu atakuwa na wasiwasi juu ya kutimiza haki anazodaiwa na mtu mwingine na kuulizwa Siku ya Qiyaamah.

Imam Abu Hanifa (rahimahullah) Na Majusi (Muabudu Moto).

Yafuatayo ni tukio la Imaam Abu Hanifah (rahimahullah) ambalo linaonyesha sifa kubwa ya amaanah ikiwa moyoni mwake na athari kubwa iliyokuwa nayo kwa huyo majusi.

Imam Abu Hanifa (rahimahullah) wakati fulani alikuwa anadaiwa kiasi cha mali na majusi fulani. Imaam Abu Hanifah (rahimahullah) alipokwenda kwenye nyumba ya majusi kuomba malipo na akafika mlangoni, kisha kwa bahati mbaya, alikanyaga uchafu uliokuwa chini, na kuufanya kushikamana na kiatu chake.

Imaam Abu Haniyfah (rahimahullah) kisha akatikisa kiatu ili kuondoa uchafu. Hata hivyo, hii ilisababisha uchafu huo kuanguka kwenye ukuta wa nyumba ya majusi.

Imaam Abu Hanifah (rahimahullah) alikuwa na wasiwasi mkubwa na kufadhaika. Alihisi kwamba ikiwa ataacha uchafu kwenye ukuta, ungesababisha ukuta kuonekana vibaya, na ikiwa angeuondoa, basi sehemu fulani ya mchanga wa ukuta pia itaondolewa, na hivyo kuharibu ukuta. Katika hali hii ya wasiwasi, Imaam Abu Hanifah (rahimahullah) aligonga mlango.

Majusi alipotoka kukutana na Imam Abu Hanifah (rahimahullah), alikuwa na wasiwasi kwamba Imam Abu Hanifah (rahimahullah) amekuja kuchukua pesa zilizobakia, na hivyo akaanza kutoa udhuru.

Hata hivyo, Imaam Abu Hanifah (rahimahullah) akamwambia, “Tuna tatizo hapa ambalo ni muhimu sana kuliko pesa unazonidai. Kwa bahati mbaya, uchafu kutoka kiatu changu ulikuja kwenye ukuta wako. Nina wasiwasi ni jinsi gani nitaweza kuusafisha bila kusababisha uharibifu wowote kwenye ukuta wako.”

Wakati yule majusi alipoiona tabia ya Imaam Abu Hanifah (rahimahullah) na sifa yake ya amaanah ndani yake, aliathirika sana na akasema, “Kabla ya kuusafisha ukuta, nataka kuutakasa moyo wangu na maisha yangu kwa kusilimu. Akisema hivi, yeye mara moja akaleta Imaan na akasilimu.

Allah Ta’ala aubariki ummah na sifa ya amaanah katika kila nyanja ya maisha yao.

About admin

Check Also

Swalaah – Ufunguo wa Jannah

Uislamu ndio njia pekee inayoongoza kwenye mapenzi ya Allah Ta’ala na inaongoza kwenye Jannah. Kupitia …