Sunna na Adabu

Njia Za Sunna Za Kufanya Udhu – Sehemu Ya Nane

24. Usitumie maji vibaya ukiwa unafanya udhu.

Sayyidina Abdullah Bin Amr (radhiyallahu anhu) ameripoti kwamba Nabii wa Allah (sallallahu alaih wasallam) alipita kwa Sayyidina Sa'd (radhiyallahu anhu) akiwa anafanya udhu. Nabii wa Allah (sallallahu alaih wasallam) alimuuliza, "huu uharibifu ni wanini (ya maji kwenye udhu wako)?" Alijibu, "kwani kuna uharibifu kwenye udhu?" Nabii wa Allah (sallallahu alaih wasallam) alimjibu, "ndiyo hata kama unafanya udhu ukingoni mwa mto (pia, kuwa makini kutoharibu maji).

Soma Zaidi »

Njia Za Sanna Za Kufanya Udhu -Sehemu Ya saba

20. Osha viungo vya upande wa kulia kabla viungo vya upande wa kushoto.[1] عن أبي هريرة رضي الله عنه قال قال رسول الله صلى الله عليه وسلم إذا لبستم وإذا توضأتم فابدءوا بأيامنكم (سنن أبي داود، الرقم: ٤١٤١)[2] Sayyiduna Abu Hurairah (radhiyallahu anhu) ameripoti kwamba Sayyiduna Rasulullah (sallallahu alaih wasallam) …

Soma Zaidi »

Sunna Na Adabu Za Ramadhaani 5

27. Kaa kwenye itikafu siku 10 za mwisho za ramadhaani kama unauwezo.

Sayyidina Ibnu Abbaas (radhiyallahu ‘anhu) ameripoti kwamba Nabii wa Allah (sallallahu ‘alaihi wasallam) alisema kuhusu mwenye kukaa itkafu, "mwenye kukaa itkafu (ndani ya msikiti) anajiepusha na madhambi, na kwa wakati wote, anapata thawabu ya kufanya ibada mbali mbali angekuwa na uwezo wa kuzifanya kama asingekuwa kwenye itkafu".

Soma Zaidi »