Fadhila za Muaddhin

Adhaan ni miongoni mwa sifa muhimu za Deen za kiislaam. Uislamu umetoa heshima kubwa kwa wale wote ambao wanatoa adhaan, wakiita watu kuelekea kuswali. Siku ya qiyaamah, watu watawapongeza wale ambao walikuwa wakitoa adhaan ulimwenguni kwa sababu ya nafasi yao tukufu na hadhi ya juu aakhera. Hadithi nyingi zinataja fadhila kubwa na faida kubwa zilizohifadhiwa kwa wale ambao hutoa adhaan.

1. Muaddhin atafurahia nafasi tukufu siku ya qiyaamah.

فعن معاوية رضي الله عنه قال: سمعت رسول الله صلى الله عليه وسلم يقول: المؤذنون أطول الناس أعناقا يوم القيامة (صحيح مسلم، الرقم: ٣٨٧)

Sayyidina Mu’aawiyah (radhiyallahu ‘anhu) anaripoti, “Nimemsikia Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) akisema, ‘hakika muadhin watakuwa na ‘shingo ndefu zaidi’ siku ya qiyaamah.”

Katika hadithi hii, maana halisi ya kuwa na ‘shingo ndefu zaidi’ haikusudiwi. Badala maana ya kuwa na ‘shingo ndefu zaidi’ ni kwamba watachukua nafasitukufu za heshima.

2. Muadhin watakuwa kwenye milima ya miski siku ya qiyaamah.

فعن عبد الله بن عمر رضي الله عنهما قال قال رسول الله صلى الله عليه وسلم ثلاثة على كثبان المسك أراه قال يوم القيامة يغبطهم الأولون والآخرون رجل ينادي بالصلوات الخمس في كل يوم وليلة ورجل يؤم قوما وهم به راضون وعبد أدى حق الله وحق مواليه (سنن الترمذي، الرقم: ٢٥٦٦، وقال: هذا حديث حسن غريب)

Sayyidina Abdullah Bin Umar (radhiyallahu ‘anhu) anaripoti kuwa Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) alisema, “vikundi vitatu vya watu vitakuwa kwenye milima ya miski (siku ya qiyaamah), na watu waliopita na wa mwisho watatamani nafasitukufu zao. Wa kwanza ni mtu ambaye alikuwa akiita adhaan kila siku kwa swala tano za kila siku . Wa pili ni mtu aliyewaongoza watu katika salaah wakati walikuwa wakifurahishwa naye (yaani alitimiza wajibu wa swala kwa njia zake sahihi). Wa tatu ni mja aliyetimiza haki za Allah subhaana wata’ala na haki za mkuu wake.”

3. Kuna malipo makubwa yaliyoko akhera kwa wale wanao toa adhaan.

فعن أبي هريرة رضي الله عنه أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال لو يعلم الناس ما في النداء والصف الأول ثم لم يجدوا إلا أن يستهموا عليه لاستهموا (صحيح البخاري، الرقم: ٦١٥)

Sayyidina Abu Hurairah (radhiyallahu ‘anhu) anaripoti kuwa Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) alisema, “ikiwa watu wangejua tu thawabu kubwa ya kutoa adhaan na kuswali kwenye safa ya kwanza, na baadaye hawakuweza kupata njia ya kuamua ni nani atapewa heshima hiyo badala ya kupiga kura, dhahiri wangeweza kupiga kura kwa ajili ya kuamua.”

About admin

Check Also

Sunna Na Adabu Za Dua 8

19. Jiepushe na ulaji wa haramu au chakula chenye mashaka na kujihusisha na madhambi. Mtu …