Watu katika mikusanyiko ya salaam wanafunikwa na rehema za Allah subhaana wata’ala

عن أنس رضي الله عنه عن النبي صلى الله عليه وسلم قال: إن لله سيارةً من الملائكة يطلبون حِلَقَ الذِّكْر، فإذا أتوا عليهم حفُّوا بهم، ثم بَعثوا رائدَهم إلى السماء إلى ربّ العزة تبارك وتعالى، فيقولون: ربنا أتينا على عباد من عبادك يعظِّمون آلاءك، ويتْلُون كتابك، ويصلّون على نبيك صلى الله عليه وسلم، ويسألونك لآخرتهم وديناهم، فيقول تبارك وتعالى: غَشُّوهم رحمتي، فيقولون يا رب إن فيهم فلانًا الخَطَّاء إنما اغْتَبَقَهم اغتباقا، فيقول تبارك وتعالى: غشّوهم رحمتي، فهم الجلساءُ لا يشقى بهم جليسهم (مسند البزار، الرقم: ٦٤٩٤، وسنده حسن كما في القول البديع صـ ٢٦٧)

Anas (radhiyallahu ‘anhu) anaripoti kuwa Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) alisema, “kuna kundi la malaika wa Allah subhaana wata’ala ambao wanaendelea kuzunguka kote ulimwenguni, wakitafuta mikusanyiko ya dhikr (mikusanyiko ya kumkumbuka Allah subhaanawata’ala). Wanapopata mkusanyiko kama huo, wanakusanyika karibu nao, na baada ya hapo wanatuma wamalaaika wambele miongoni mwao mbinguni (kuripoti kwa Allah subhaana wata’ala). malaika hawa wanamwambia Allah subhaana wata’ala, “Ewe Mola wetu tulifika kwenye kundi la waja wako ambao wanachukulia neema zako kama neema kubwa juu yao, wanasoma kitaabu chako, wanatuma salaam kwa Nabii wako (sallallahu ‘alaihi wasallam) na wanakuomba kwa mahitaji yao yanayohusiana na aakhera na dunia.” Allah subhaana wata’ala Atajibu “wazungushie kwa rehema zangu.” Malaika kisha huwasilisha, “ewe Mola! kati yao kuna flani na flani ambae ametenda madhambi mengi, na amefika tu mwisho wa mkusanyiko. Allah subhaana wata’ala atasema, “wafunike watu wote wa mkusanyiko huo (pamoja na yeye) kwa rehema zangu, kwa sababu watu katika mkusanyiko huu ni kama kwamba hakuna mtu yoyote anayejiunga nao atakuwa na bahati mbaya ya kunyimwa rehema zangu.”

Kuandika “sallallahu ‘alaihi wasallam” kwa ukamilifu

Sayyidina Ubaidullah Bin Umar Qawaareeri (rahimahullah) alisema:

Nilikuwa na rafiki wa karibu ambaye alikuwa mwandishi wakitaalama. Baada ya kufariki, niliwahi kumuona kwenye ndoto na kumuuliza ni vipi Allah subhaana wata’ala alishughulika nawe. Alijibu kuwa Allah subhaana wata’ala amemsamehe.

Nilipomuuliza sababu, akasema, “ilikuwa tabia yangu wakati wa uhai wangu kwamba kila nilipoandika jina tukufu la Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam), siku zote niliandika ‘sallallahu ‘alaihi wasallam’ baada ya jina lake. Allah subhaana wata’ala alipenda kitendo hiki sana hivi kwamba amenipa fadhila ambazo hakuna jicho limewahi kuona, wala sikio lolote lililowahi kusikia, na wala mawazo ya neema kama hizo hayakuwahi kuvuka akili ya mtu yoyote.”(Al-Qawlul Badee, Pg, 486)

About admin

Check Also

Chanzo cha nuru siku ya Qiyaama

عن ابن عمر رضي الله عنهما قال قال رسول الله صلى الله عليه وسلم زينوا …