Fadhila za Muaddhin 2

4.kila kiumbe (kama jini, mwanadamu au kiumbe mwingine yoyote) ambaye husikia sauti ya muadhin akiadhini adhaan atashuhudia kwa niaba yake siku ya qiyaamah.

فعن عبد الرحمن بن عبد الله بن عبد الرحمن بن أبي صعصعة الأنصاري ثم المازني عن أبيه أنه أخبره أن أبا سعيد الخدري رضي الله عنه قال له إني أراك تحب الغنم والبادية فإذا كنت في غنمك أو باديتك فأذنت بالصلاة فارفع صوتك بالنداء فإنه لا يسمع مدى صوت المؤذن جن ولا إنس ولا شيء إلا شهد له يوم القيامة قال أبو سعيد سمعته من رسول الله صلى الله عليه وسلم (صحيح البخاري، الرقم: ٦٠٩)

Imeripotiwa kuhusu sayyidina Abdullah bin abdir rahmaan bin Abi sa’sa’ah (rahimahullah) kwamba wakati mmoja, sayyidina Abu Sa’eed khudri (radhiyallahu ‘anhu) alimwambia, “Ninaona kama unapenda kubaki na mifugo yako (ukizifuga) uwanjani. Wakati uko kati ya mifugo zako au uwanjani, (na muda wa swalaah ukaingia) na unatamani kutoa adhaan, basi unapaswa kupaza sauti yako na kuita adhaan, kwa hakika majini, wanadamu au viumbe vingine vyote ambao husikia sauti ya muadhin mahali popote watashuhudia kwa niaba yake siku ya qiyaamah.” Sayyidina Abu Saeed (radhiyallahu ‘anhu) alisema, “Nimesikia hii kutoka kwa Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam).”

5. Msamaha umetangazwa kwa muadhin. Vile vile, habari njema zimetolewa kuhusu muadhin kwamba amebarikiwa na thawabu ya wale wote waliyo kuja kuswali kutokana na kuitikia adhaan yake.

فعن البراء بن عازب رضي الله عنه أن نبي الله صلى الله عليه وسلم قال إن الله وملائكته يصلون على الصف المقدم والمؤذن يغفر له بمد صوته ويصدقه من سمعه من رطب ويابس وله مثل أجر من صلى معه (سنن النسائي، الرقم: ٦٤٥، وإسناده حسن جيد كما في الترغيب والترهيب للمنذري ١/٢٤٣)

Sayyidina Baraa Bin Aazib (radhiyallahu ‘anhu) anaripoti kuwa Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) alisema, “hakika Allah subhaana wata’ala huonyesha huruma yake maalum kwa wale (ambao hutekeleza swala) katika saff ya kwanza na malaika hufanya dua maalum kwao. muadhin atapata msamaha kutoka kwa Allah subhaana wata’ala kwa umbali wa sauti yake inako sikika (ikiwa alikuwa na madhambi mengi ambayo hufunika umbali kutoka mahali anapoita adhaan hadi mahali sauti yake inapofikia, dhambi hizo zote zitasamehewa, au kwa muda wote itachukua sauti yake kufikia hatua kubwa zaidi, atapokea msamaha wa Allah subhaana wata’ala kwa ule muda ulimchukua kufanya madhambi ndani ya maisha yake), na kila kiumbe kiwe na uhai au la, atashuhudia kwa niaba yake (siku ya qiyaamah), na atapokea tuzo ya wale watu wote wakitaalama swalaah pamoja naye ( yaani wale watu wote walioswali kwa sababu ya kusikia adhaan yake).”

About admin

Check Also

Sunna Na Adabu Za Dua 8

19. Jiepushe na ulaji wa haramu au chakula chenye mashaka na kujihusisha na madhambi. Mtu …