Malaika wakimiminika kwenye mikusanyiko ya Dhikr

عن عقبة بن عامر رضي الله عنه قال : قال رسول الله صلى الله عليه وسلم : إن للمساجد أوتادا جلساؤهم الملائكة إن غابوا فقدوهم وإن مرضوا عادوهم وإن رأوهم رحبوا بهم وإن طلبوا حاجة أعانوهم فإذا جلسوا حفت بهم الملائكة من لدن أقدامهم إلى عنان السماء بأيديهم قراطيس الفضة وأقلام الذهب يكتبون الصلاة على النبي صلى الله عليه وسلم ويقولون : اذكروا رحمكم الله زيدوا زادكم الله فإذا استفتحوا الذكر فتحت لهم أبواب السماء واستجيب لهم الدعاء وتطلع عليهم الحور العين وأقبل الله عز وجل عليهم بوجهه ما لم يخوضوا في حديث غيره ويتفرقوا فإذا تفرقوا أقام الزوار يلتمسون حلق الذكر (القربة لابن بشكوال، الرقم: 115، وسنده ضعيف كما في القول البديع صـ 257)

Sayyidina Uqbah Bin Aamir (radhiyallahu ‘anhu) anaripoti kwamba Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) amesema, “hakika misikiti ina ‘vigingi’ (yaani watu wanaoswalia katika misikiti, wakijishughulisha na ibaadah, kama vile vigingi vinavyowekwa ardhini). Malaika wanabaki kukaa pamoja na watu kama hao, ikiwa hawapo katika Misikiti, Malaika huwa wanawakumbuka, nawakiwa wagonjwa, Malaika huwatembelea, na Malaika wakiwaona huwakaribisha, na wakiwa na haja, Malaika huwa wakiwasaidia kuwatimizia haja zao. Wanapokuwa wamekaa (misikitini kwa ajili ya kumkumbuka Allah subhaana wata’ala kumswalia Nabii wa Allah subhaana wata’ala n.k.), Malaika huwazunguka kutoka miguu yao mpaka mbinguni. Malaika wana karatasi za fedha na kalamu za dhahabu mikononi mwao ambao wanarikodi swala na salamu za Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) (inayosomwa na watu hao). Malaika huwaambia, “Endeleeni kujishughulisha na Dhikri ya Allah subhaana wata’ala, Allah subhaana wata’ala akurehemuni! Zidisheni (Dhikri na salaam zenu), Allah subhaana wata’ala akuzidishieni (katika wema)!”watu hawa wanapoanza kufanya Dhikri ya Allah subhaanawata’ala, milango ya mbingu inafunguliwa kwa ajili yao, na kujibiwa Dua zao, mahuur wa jannah wanawachungulia, na Allah subhaana wata’ala Anawatumia rehma zake maalum juu Yao kama hawajishughulishi na kazi zingine na hawaondoki. Wakiondoka Malaika wanainuka na kutafuta mikusanyiko ya Dhikr.”

Kuchukua tahadhari kwa kuandika salaam.

Sayyidina Abu Sulaimaan, Muhammad Bin Husain (rahimahullah) anasema:

Miongoni mwa majirani zangu alikuwepo mtu mmoja kwa jina la Fadhl ambaye alikuwa akijishughulisha katika kuswali nafl na kufunga nafl.

Aliwahi kunitajia, “Nilikuwa nikinakili hadithi za Nabii wa Allah subhaana wata’ala lakini sikuwa na tabia ya kuandika swala na salaam baada ya jina la Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) Nabi wa Allah subhaana wata’ala alinijia ndotoni na akaniambia “Kwa nini unashindwa kunisomea salaam kila wakati jina langu linaposemwa au kuandikwa?”

Fadhl basi akachukua tahadhari kubwa katika kusoma salaam juu ya Nabii wa Allah (sallallahu ‘alaihi wasallam) kila linapotajwa jina la Rasulullah. Siku chache baadaye alimuona Nabii wa Allah subhaana wata’ala tena katika muono na akamwambia, “Endelea kunisomea salaam kila linapotajwa jina langu, kwa hakika salaam zako zinanifikia.” (Al Qawlul Badee, Pg, 487)

About admin

Check Also

Chanzo cha nuru siku ya Qiyaama

عن ابن عمر رضي الله عنهما قال قال رسول الله صلى الله عليه وسلم زينوا …