6. Muadhin ameelezwa kwenye Hadithi kuwa amehesabiwa kuwa waja bora wa Allah subhaana wata’ala.
فعن ابن أبي أوفى رضي الله عنه قال قال رسول الله صلى الله عليه وسلم إن خيار عباد الله الذين يراعون الشمس والقمر والنجوم والأظلة لذكر الله (المستدرك على الصحيحين للحاكم، الرقم: ١٦٣، وإسناده صحيح كما قال الذهبي في التلخيص)
Sayyidina Ibnu Abi Awfaa (radhiyallahu ‘anhu) anaripoti kuwa Nabii wa Allah (sallallahu ‘alaihi wasallam) amesema, “hakika waja bora wa Allah subhaana wata’ala ni wale wanaozingatia (kuchomoza na kuzama kwa) jua, na mwezi, na nyota, na urefu wa ) vivuli vya ajili ya kumkumbuka ya Allah subhaana wata’ala (yaani wanatimiza ibaadah zao kwa wakati maalum kwa mujibu wa amri ya Allah subhaana wata’ala, huku akichunga wakati kwa kuangalia jua, mwezi, nyota na urefu wa vivuli kama ilivyoelezwa katika Hadithi. Muadhin amehesabiwa katika bashara hii kwa sababu ya yeye kuchunga wakati ili aweze kutoa adhana ya kila Swalaah kwa wakati wake).
7. Uhuru na moto wa Jahannam umeahidiwa kwa mwenye kutoa adhana kwa muda wa miaka saba.
فعن ابن عباس رضي الله عنهما أن النبي صلى الله عليه وسلم قال من أذن سبع سنين محتسبا كتبت له براءة من النار (سنن الترمذي، الرقم: ٢٠٦، وسكت عنه الحافظ في الفصل الثاني من هداية الرواة (١/٣١٨) فلا تقل درجته عن الحسن عنده)
Sayyidina Ibnu Abbaas (radhiyallahu ‘anhuma) anaripoti kwamba Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) amesema, “Mwenye kutoa adhana kwa miaka saba kwa ikhlasi na matumaini ya kupata malipo anapata dhamana ya uhuru kutoka kwa moto wa Jahannam.”
8. Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) aliwafanyia dua na msamaha Kwa wale wanao toa adhana.
فعن أبى هريرة رضي الله عنه قال قال رسول الله صلى الله عليه وسلم الإمام ضامن والمؤذن مؤتمن اللهم أرشد الأئمة واغفر للمؤذنين (سنن أبي داود، الرقم: ٥١٧، وسكت عنه الحافظ في الفصل الثاني من هداية الرواة (١/٣١٨) فلا تقل درجته عن الحسن عنده)
Sayyidina Abu Huraira (radhiyallahu ‘anhu) anaripoti kuwa Nabii wa Allah subhaana wata’ala amesema, “Imaam anawajibika (kwa Swalaah ya jamaa nzima) na muadhin ni yule aliyekabidhiwa amana (yaani amekabidhiwa jukumu la kulingania adhana kwa wakati wake). Ewe Allah subhaana wata’ala, waongoze maimamu.(kuelekea kutimiza wajibu wao wa kuswali kwa usahihi) na umsamehe muadhini (kwa mapungufu yao)”.