Bahili wa kweli

عن حسين بن علي بن أبي طالب قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: البخيل الذي من ذكرت عنده فلم يصل علي (سنن الترمذي، الرقم: 3546، وقال هذا حديث حسن صحيح غريب)

Sayyidina Husain (radhiyallahu ‘anhu) anaripoti kwamba Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) alisema, “bakhili wa kweli ni yule ambaye jina langu linatajwa mbele yake, lakini hanitumii salamu.”

Kushindwa kuandika salamu juu ya Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam)

Sayyidina Hasan bin Moosa Al-Had rami (rahimahullah) , ambaye anajulikana sana kama Ibnu Ujainah (rahimahullah) anaeleza:

Nilikuwa nikiandika hadithi na kwa kuharakisha kwangu nilikuwa nikisahau kuandika Salaat na salaam juu ya Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) mahali ambapo jina la Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) Limeandikwa. Baada ya hapo, nilimuona Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) katika ndoto. akaniambia, “vipi unashindwa kuandika Salaat na salaam kwenye jina langu kama jinsi Abu Amr Tabari (rahimahullah) anafanya?

Nilipoamka, nilihisi kufedheika sana na kujawa na uchungu na mara moja nikafanya azimiyo kwamba siku zijazo, wakati wowote ninapoandika hadithi yoyote hakika nitaandika “(sallallahu ‘alaihi wasallam)”. (Al Qawlul Badee, Pg 492)

About admin

Check Also

Chanzo cha nuru siku ya Qiyaama

عن ابن عمر رضي الله عنهما قال قال رسول الله صلى الله عليه وسلم زينوا …