Fadhila za Muaddhin

9. Ilikuwa ni matamanio ya sahaaba (radhiyallahu ‘anhum) kutoa adhana na walitamani watoto wao pia watoe adhana.

Chini kuna baadhi ya hadithi zinazoonyesha shauku ya sahaaba (radhiyallahu ‘anhum) kutoa adhaan:

Hamu ya Sayyidina Ali (radhiyallahu ‘anhu) kwa Sayyidina Hasan (radhiyallahu ‘anhu) na Sayyidina Husein (radhiyallahu ‘anhu) kutoa adhana:

عن علي رضي الله عنه قال ندمت أن لا أكون طلبت إلى رسول الله صلى الله عليه وسلم فيجعل الحسن والحسين مؤذنين (مجمع الزوائد، الرقم: ١٨٣٦)

Imepokelewa kwamba Sayyidina Ali (radhiyallahu ‘anhu) alisema, “Ninajuta juu ya ukweli kwamba sikumuomba Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) kuwaweka wanangu wawili, Hasan na Husein (radhiyallahu ‘anhuma) kama muadhini wa kutoa adhaan.”

Shauku ya Sayyidina Umar (radhiyallahu ‘anhu) kutowa adhana:

عن قيس بن أبي حازم قال قدمنا على عمر بن الخطاب فسأل من مؤذنكم فقلنا عبيدنا وموالينا فقال بيده هكذا يقلبها عبيدنا وموالينا إن ذلكم بكم لنقص شديد لو أطقت الأذان مع الخلافة لأذنت (السنن الكبرى للبيهقي، الرقم: ٢٠٠٢)

Qais bin Abi Haazim (rahimahullah) anaripoti, “wakati mmoja tulikuja (madina munawwara) kukutana na Umar (radhiyallahu ‘anhu) Wakati wa mazungumzo yetu alituuliza, ‘nani anatoa adhana katika sehemu unayoishi?’ Tukajibu: Tumewaweka watumwa wetu kutoa adhana. Umar (radhiyallahu ‘anhu) aliashiria kwa mikono yake (kwa mshangao akirudia maneno yetu) akisema, ‘tumewaweka watumwa wetu ili watoe adhaan.’ Kisha akasema: Hakika huu ni upungufu mkubwa kwenu (kwamba umechagua watu kama hao kutoa adhana watu wasio na elimu ya Dini). (adhana ni ibaada kubwa na malipo yake ni mengi mno kiasi kwamba) lau ningelingania kutoa adhana pamoja na kusimamia mambo ya khilaafah, bila shaka ningekubali nafasi ya muadhin na ningeita adhana.”

وعن عمر رضي الله عنهما أنه قال لو كنت مؤذنا لكمل أمري وما باليت أن لا أنتصب لقيام ليل ولا لصيام نهار سمعت رسول الله صلى الله عليه وسلم يقول اللهم اغفر للمؤذنين ثلاثا قلت يا رسول الله تركتنا ونحن نجتلد على الأذان بالسيوف فقال كلا يا عمر إنه سيأتي زمان يتركون الأذان على ضعفائهم تلك لحوم حرمها الله على النار لحوم المؤذنين (كشف الخفاء، الرقم: ٢١١٨)

Imepokewa kuhusu Sayyidina Umar (radhiyallahu ‘anhu) kwamba amesema, “Lau ningeliweza kutoa adhana (pamoja na kusimamia mambo ya khilaafah), bila shaka furaha yangu ingekamilika. (malipo ya kutoa adhana ni makubwa kiasi kwamba kama ningejaliwa na heshima ya kuwa muadhin na ) kama nisinge swali nafili yoyote usiku (tahajjud) au kufunga nafl wakati wa mchana, lisinge nihuzunisha. Nilimsikia Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) akiwaombea dua maalum wa Muadhini wa Ummah huu akisema, ‘Ewe Allah subhaana wata’ala, wasamehe madhambi ya Muadhin!’ Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) alifanya dua hii mara tatu. kwa mshangao nikasema, ‘Ewe Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam).(Umepandisha cheo cha muadhini kiasi kwamba) sasa umetuacha katika hali ya kuwa tutakuwa tayari kupigana baina yetu kutumia vipanga vyetu ili kutoa adhana.’ Nabii wa Allah (sallallahu ‘alaihi wasallam) akasema, ‘Hapana, ewe Umar (radhiyallahu ‘anhu)! Utafika wakati ambapo hamu ya kuita adhana haitakuwa tena katika nyoyo za watu, kiasi kwamba watu watategemea wanyonge miongoni mwao kutoa adhana. Hao watu (wa Muadhin) Allah subhaana wata’ala amefanya moto wa Jahannam kuwa haramu juu ya miili yao, miili ya muadhin.”

About admin

Check Also

Maneno ya Iqaamah na Njia ya Sunnah ya kutoa Iqaamah

1. Maneno ya iqaamah ni sawa sawa na maneno ya adhaan. Kwa hivyo, wakati wa …