Dalili ya kuwa na tabia mbaya na kutokuwa na shukrani.

عن قتادة قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: من الجفاء أن أذكر عند الرجل فلا يصلي علي (الإعلام بفضل الصلاة على النبي صلى الله عليه وسلم للنميري، الرقم: 209، ورواته ثقات كما في القول البديع صـ 311)

Sayyidina Qataadah (rahimahullah) anaripoti kwamba Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) amesema, “ni dalili ya mtu kuwa na tabia mbaya (na kukosa shukurani) kwamba jina langu linatajwa mbele yake, lakini anapuuzia kunitumia salamu.”

Kufikia nafasi ya juu kwa kuandika salaa na salaam Kwa wingi

Sayyidina Ja’far Bin Abdullah (rahimahullah) anaeleza:

Katika tukio moja, nilimuona Imaam Abu Zur’ah (rahimahullah) (mwanachuoni mashuhuri wa Hadith) katika ndoto. Nilimuona mbinguni akiwaongoza malaika Katika swala.

Nilimuuliza, “Ewe Abu Zur’ah, umefikaje nafasi hii ya juu ya heshima?”akajibu, “kwa mkono wangu huu, nimeandika hadithi milioni moja, na kila nilipoandika jina lililobarikiwa la Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) pia niliandika salaa na salaam, na Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) kasema, ‘yoyote anayenitumia salaam mara moja Allah subhaana wata’ala atamrehemu mara kumi.”

Kwa mujibu wa hesabu hii, itamaanisha kwamba (kupitia yeye kuandika salaa na salaam mara milioni moja), rehema kutoka kwa Allah subhaana wata’ala zingefikia milioni kumi juu yake. Mtu anaweza kufikiria vizuri kwamba wakati rehema moja tu kutoka upande wa Allah subhaana wata’ala ni ya thamani zaidi kuliko kila kitu duniani, basi Kwa kiasi gani atabahatika yule ambaye rehema milioni kumi za Allah subhaana wata’ala zitamshukia! (Al-Qawlul Badee, Pg, 489)

About admin

Check Also

Chanzo cha nuru siku ya Qiyaama

عن ابن عمر رضي الله عنهما قال قال رسول الله صلى الله عليه وسلم زينوا …