Njia ya Sunna ya kuita adhana

1. Hakikisha kwamba nia yako ya kuita adhaan ni kumridhisha Allah subhaana wata’ala pekee yake.

فعن ابن عباس رضي الله عنهما أن النبي صلى الله عليه وسلم قال من أذن سبع سنين محتسبا كتبت له براءة من النار (سنن الترمذي، الرقم: ٢٠٦)[1]

Sayyidina Ibnu Abbas (radhiyallahu ‘anhuma) anaripoti kwamba Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) kasema, “mwenye kuita adhana kwa miaka saba kwa ikhlaasi na matumaini ya kupata malipo anapata dhamana ya uhuru kutokana na moto wa jahannam.”

2. Kuita adhaan kwa wakati wake.

فعن أبي محذورة رضي الله عنه قال قال رسول الله صلى الله عليه وسلم أمناء المسلمين على صلاتهم وسحورهم المؤذنون (السنن الكبرى للبيهقي، الرقم: ١٩٩٩)[2]

Sayyidina Abu Mahzoorah (radhiyallahu ‘anhu) anaripoti kuwa Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) amesema, “wasimamizi wa Waislamu juu ya swala na daku zao ni waadhiin (yaani watoa adhana wamepewa jukumu la kuwatahadharisha Waislamu juu ya wakati sahihi wa Swalaah na wakati wa daku.)”

3. Kuita adhaan nje ya msikiti, ikiwezekana kutoka mahali palipoinuka ili sauti iweze kufika mbali zaidi.[3]

فعن عروة بن الزبير عن امرأة من بني النجار قالت كان بيتي من أطول بيت حول المسجد وكان بلال يؤذن عليه الفجر فيأتي بسحر فيجلس على البيت ينظر إلى الفجر فإذا رآه تمطى ثم قال اللهم إني أحمدك وأستعينك على قريش أن يقيموا دينك قالت ثم يؤذن قالت والله ما علمته كان تركها ليلة واحدة تعني هذه الكلمات (سنن أبي داود، الرقم: ٥١٩)[4]

Sayyidina Urwah bin Zubair (rahimahullah) anaripoti kwamba mwanamke kutoka kabila la Banu Najjaar anaeleza, “Nyumba yangu ilikuwa moja ya nyumba za juu kabisa kuzunguka msikiti(Musjid un Nabawi), na Bilaal (radhiyallahu ‘anhu) alikua akitoa adhaan juu ya nyumba yangu. alikua akifika wakati wa daku na kukaa juu ya paa ya nyumba, na kuangalia mawingu na kusubiri wakati wa fajr kuingia. Pindi aonapo muda umeingia, alijinyoosha (kutokana na kukaa muda mrefu, akingoja kuona wakati wa alfajiri) na kufanya dua ifuatayo, ‘Ewe Allah subhaana wata’ala nakusifu (kwa kuniruhusu kutoa adhaan). Naomba msaada wako na nakuomba uwaongoze Maquraish (familia ya Nabii wa Allah subhaana wata’ala ambayo walikuwa bado hawajasilimu) katika Uislamu ili wasimamie na wasimamishe Dini yako (duniani).”‘ Wanawake wakasema zaidi, “basi baada ya hapo ataita adhaan. Ninakula kiapo kwa jina la Allah subhaana wata’ala sina kumkumbuka akiacha dua yake hata siku moja (yaani dua yake kwa maquraishi kabla ya kuita adhana)”.


[1] قال أبو عيسى: حديث ابن عباس حديث غريب

[2] عن الحسن أن النبي صلى الله عليه وسلم قال المؤذنون أمناء المسلمين على صلاتهم قال وذكر معها غيرها وهذا المرسل شاهد لما تقدم (السنن الكبرى للبيهقي، الرقم: 2000)

عن الحسن أن النبي صلى الله عليه وسلم قال المؤذنون أمناء الناس على صلاتهم (لأن الناس متى سمعوا الأذان أدوا الفريضة اعتمادا عليه والغرض من الحديث إشعار المؤذنين بمسؤليتهم ليحتفلوا بها ويتحروا الأوقات حتى لا يضلوا الناس ويحملوهم على الصلاة قبل وقتها) وذكر معها غيرها (مسند الشافعي، الرقم: 173)

[3] قال أصحابنا رحمهم الله يستحب أن يكون الأذان بقرب المسجد (المجموع شرح المهذب 3/95)

والمستحب أن يكون على موضع عال لأن الذي رآه عبد الله بن زيد كان على جذم حائط ولأنه أبلغ في الإعلام (المجموع شرح المهذب 3/79)

ويستحب … أن يؤذن على موضع عال من منارة أو سطح ونحوهما (روضة الطالبين 1/313)

[4] قال الحافظ أخرجه أبو داود وإسناده حسن (فتح الباري 2/121)

About admin

Check Also

Sunna Na Adabu Za Dua 8

19. Jiepushe na ulaji wa haramu au chakula chenye mashaka na kujihusisha na madhambi. Mtu …