Abu Hurairah (radhiyallahu ‘anhu) anaripoti kuwa Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) anasema, "yule anayetaka salamu yake juu yangu ipimwe kwa kiwango kilicho pimwa kamili (na hivyo kupokea tuzo kamili kwa salaam) wakati akisoma salaam juu yetu, na ahlul bayt, basi anapaswa kusoma salaam ifuatayo:
Ewe Allah subhaanawata'ala! tuma salaamu kwa Nabii Muhammad (sallallahu ‘alaihi wasallam) Nabii asiye juwa kusoma, wake zake, mama wa waumini, kizazi chake na watu wa nyumba yake kama jinsi ulivyotuma salaamu kwa familia ya Ebrahim (alahis salaam), hakika wewe ndiye unastahili sifa, mwingi wa kupandisha.
Soma Zaidi »