Sayyidina Samurah Suwaai (radhiallahu anhu), baba wa Sayyidina Jaabir (radhiallahu anhu), ameripoti kwamba: tuliwahi kuwa na Nabii wa Allah (sallallahu alaihi wasallam) pindi mtu mmoja alikuja kwa Nabii wa Allah (sallallahu alaihi wasallam) na akauliza, " ewe Nabii wa Allah (sallallahu alaihi wasallam) !ni tendo gani linalomrizisha Allah subhaana wata'alah zaidi?" Nabii wa Allah-(sallallahu alaihi wasallam) akajibu, "maneno ya ukweli na kutimiza uwaminifu." Nikasema, "ewe Nabii wa Allah (sallallahu alaihi wasallam)! Nakuomba utuzidishie nasaha (kuhusu matendo yanayo mrizisha Allah subhaana wata'alah)!" Nabii wa Allah (sallallahu alaihi wasallam) akasema, " swali wakati wa usiku na funga wakati wa jua kali." Kisha nikasema, ewe Nabii wa Allah (sallallahu alaihi wasallam)! Nakuomba utuzidishie nasaha!" Nabii wa Allah (sallallahu alaihi wasallam) akasema, " jishughulishe na zikr kwa wingi na nitumie salaam inaondowa umasikini," nikauliza tena, ewe Nabii wa Allah (sallallahu alaihi wasallam) nakuomba utuzidishie nasaha! Nabii wa Allah (sallallahu alaihi wasallam) akasema, yule atakae swalisha watu basi afupishe swala,kwa sababu kwenye jamaa kuna wazee, kuna wagonjwa, vijana na watu kuna ambao wana dharura."
Soma Zaidi »