عن أبي هريرة رضي الله عنه قال : قال رسول الله صلى الله عليه وسلم : أكثروا الصلاة علي في الليلة الزهراء واليوم الأغر فإن صلاتكم تعرض علي (المعجم الاوسط للطبراني وسنده ضعيف لكن يتقوى بشواهده كما في القول البديع صـ 325)
Abu Hurayrah (radhiyallahu ‘anhu) anaripoti kwamba Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) kasema, “zidisheni kunitumia salaa na salaam katika usiku na siku ya Ijumaah, kwa sababu salaa na salaam zako zitaletewa kwangu.”
Kupokea Chakula Maalum
Shah Waliyullah (rahimahullah) anaandika katika Al-Hirzuth Thameen (chini ya namba kumi na tisa) ambayo baba yake alieleza yafuatayo:
Wakati fulani nilikuwa nikisafiri katika mwezi wa Ramaadhaan. Nilikuwa bado mtoto sana wakati huo na nilikuwa nikipitia na matatizo makubwa. Katika Hali hiyo, nililala na kumuona Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam).Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) alinipa chakula kitamu chenyewe wali, zafarani, sukari na samli, na nikala na nikashiba. Baada ya hapo, Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) alinipa maji ya kunywa kusababisha kiu na njaa yangu kuondoka kabisa, na nilipoamka, nilisikia harufu ya
zafarani kwenye vidole vyangu.
Maelezo: Baba yake Shah Waliyullah (rahimahullah) na familia yake walikuwa wapenzi wenye bidii wa Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) na walikuwa wakimswalia Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) kwa wingi. (Fadaail e Durood, Pg, 188)