Tafseer ya Sura Alam Nashrah

أَلَمْ نَشْرَحْ لَكَ صَدْرَكَ ﴿١﴾ وَوَضَعْنَا عَنكَ وِزْرَكَ ﴿٢﴾ الَّذِي أَنقَضَ ظَهْرَكَ ﴿٣﴾وَرَفَعْنَا لَكَ ذِكْرَكَ ﴿٤﴾ فَإِنَّ مَعَ الْعُسْرِ يُسْرًا ﴿٥﴾ إِنَّ مَعَ الْعُسْرِ يُسْرًا ﴿٦﴾ فَإِذَا فَرَغْتَ فَانصَبْ ﴿٧﴾ وَإِلَىٰ رَبِّكَ فَارْغَب.

Je! hatukukupanulia kifua chako, na tukakuondolea mzigo wako ambao ungeliweza kukuvunja mgongo wako. Na tumelitukuza utukufu wako (jina lako tukufu na cheo chako). Basi hakika kwa kila ugumu ni wepesi. Hakika kwa kila ugumu ni wepesi. Basi unapokuwa huru (katika uduma unazozitoa kwa watu), basi fanya bidii (katika ibada), na mgeukie Mola wako kwa kujipendekeza.

Wahi ulikuwa ukimteremkia Nabii (sallallahu ‘alaihi wasallam), ulikuwa mzito sana kwamba ikiwa Nabii (sallallahu ‘alaihi wasallam) alikuwa amekaa juu ya ngamia, ngamia angekaa chini kwa sababu hawezi kuumudu mzigo huo yaani  uzito wa wahi.

Akieleza ukubwa wa wahi, Allah Ta’ala anaeleza, “Lau tungeiteremsha hii Quraan (yaani wahi) juu ya mlima, unge uona ukiwa umenyenyekea na kupasuka kwa ajili ya kumcha Allah Ta’ala. ” Hata hivyo, Allah Ta’ala alikuwa amepanua kifua cha baarak cha Rasulullah (Sallallahu ‘alaihi wasallam) ili aweze kustahimili na kusimamia uzito wa wahi.

katika Aya hii, Allah Ta‘ala anaeleza kwamba Amemuondolea Nabii (Sallallahu ‘alaihi wasallam) mzigo na uzito ambao ulikuwa mzito sana mgongoni mwake hadi ungeweza kumvunja mgongo. Mzigo na uzito huu unahusu mzigo na uzito aliyo upata Nabii (Sallallahu ‘alaihi wasallam) wakati wahi unateremshwa kwake. Vile vile, inaweza pia kumaanisha uzito wa jukumu alilowekwa katika kufikisha ujumbe wa Qur-aan na Dini nzima kwa ummah mpaka Siku ya Qiyaamah. Lau isingelikuwa uingiliaji na usaidizi wa Allah Ta’ala katika kupanua kifua cha baarak cha Rasulullah (Sallallahu ‘alaihi wasallam) na kumuwezesha kustahimili uzito na jukumu hili, bila shaka isingewezekana kwake kuvumilia.

وَرَفَعْنَا لَكَ ذِكْرَكَ

Na tumelitukuza jina lako (na cheo chako).

Katika aya hii, tunaona mapenzi makubwa aliyonayo Allah Ta’ala kwa Rasulullah (Sallallahu ‘alaihi wasallam) na nafasi iliyotukuka ambayo Allah Ta’ala amemtukuza nayo. Wakati wowote jina la Allah Ta’ala linapochukuliwa, basi jina la Rasulullah (Sallallahu ‘alaihi wasallam) pia huchukuliwa kwa jina Lake.

Wakati wa kusoma kalimah na kuingia katika zizi la Uislamu, jina la Rasulullah (Sallallahu ‘alaihi wasallam) huchukuliwa pamoja na jina la Allah Ta‘ala. Katika adhaan, iqaamah na khutbah, jina mubaaraka la Rasulullah (Sallallahu ‘alaihi wasallam) limechukuliwa pamoja na jina la Allah Ta‘ala. Katika Swalah, wakati wa tashahhud, jina la Rasulullah (Sallallahu ‘alaihi wasallam) limechukuliwa pamoja na jina la Allah Ta’ala, na ikiwa jina lake halitachukuliwa na kutoswaliwa , basi Swalah bado haijakamilika. Katika Quraan Tukufu, Allah Ta’ala mara kwa mara anazungumza kuhusu Rasulullah (Sallallahu ‘alaihi wasallam) kwa heshima na upendo. Kwa namna hii, Allah Ta’ala ameitukuza heshima na sifa zake.

فَإِنَّ مَعَ الْعُسْرِ يُسْرًا ﴿٥﴾ إِنَّ مَعَ الْعُسْرِ يُسْرًا

Basi hakika kwa kila ugumu kuna wepesi. Hakika kwa kila ugumu kuna wepesi.

Allah Ta’ala ameiumba dunia hii kuwa ni sehemu ya mitihani na dhiki. Kwa hivyo, mwanadamu atakabidhiwa na changamoto na mitihani mbalimbali katika njia tofauti ndani ya maisha yake.

Kuna wakati mtu atapimwa afya yake, na kuna wakati atapimwa kwa mali zake. Kuna wakati atapimwa na watoto zake, na kuna wakati atapimwa kwa mali na vitu vyake na menginevyo. Kwa hali yoyote ile mtu anayo, hakika atapitwa na aina yoyote ya ugumu – iwe ya kimwili, kiakili au kihisia – ndani ya maisha yake . Kwa hiyo katika aya hii, Allah Ta’ala Anatufahamisha kwamba katika kila shida kuja wepesi.

Kwa hivyo, ikiwa muumini atashikamana na Dini ya Allah Ta’ala na kuwa na yakini kamili katika ahadi za Allah Ta’ala na maneno ya Mubaarak ya Rasulullah (Sallallahu ‘alaihi wasallam), hakika atapata wepesi baada ya kila shida.

فَإِذَا فَرَغْتَ فَانصَبْ ﴿٧﴾ وَإِلَىٰ رَبِّكَ فَارْغَب

Basi unapokuwa huru (katika uduma unazozitoa kwa watu), basi fanya bidii (katika ibada), na mgeukie Mola wako kwa kujipendekeza.

Katika aya hii, Rasulullah (Sallallahu ‘alaihi wasallam) anaelezwa na Allah Ta’ala na kuambiwa kwamba atakapomaliza kazi ya kuhubiri na kuuongoza ummah katika idara mbalimbali za Dini, basi aelekeze mazingatio yake kwa Mola wake na ajitahidi katika ibaadah.

Maulamaa wanaeleza kwamba wale wote wanaojishughulisha na kazi za Dini, basi kama ilivyo muhimu kwao kufundisha na kuhubiri Dini, kuwahimiza watu kuelekea katika mema na kuwaongoza kwa usahihi, vile vile pia ni muhimu kwao kufanya bidii katika ibaadah zao,kujirekebisha, kuboresha uhusiano wao na Allah Ta’ala, na kumkumbuka Allah Ta’ala kwa muda wote.

Huu ni mpango mpana – kwamba mtu anapaswa kuwa na wasiwasi juu ya maendeleo yake mwenyewe, na wakati huo huo, pia anapaswa kuwa na wasiwasi juu ya maendeleo ya Ummah. Juhudi za mtu zisiwe za upande mmoja, ambapo anajishughulisha tu na maendeleo yake na anabakia kutojali maendeleo ya Ummah, au anajali tu maendeleo ya Ummah na anabakia kutojali kuhusu maisha yake binafsi. Kwa hivyo, aya hii inatufundisha kwamba vyote hivi viwili ni muhimu.

About admin

Check Also

Tafseer Ya Surah Lahab

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ تَبَّتْ يَدَا أَبِي لَهَبٍ وَتَبَّ ‎﴿١﴾‏ مَا أَغْنَىٰ عَنْهُ مَالُهُ وَمَا كَسَبَ ‎﴿٢﴾‏ سَيَصْلَىٰ نَارًا …