عن أبي أمامة عن النبي صلى الله عليه وسلم قال: من دعا بهؤلاء الدعوات في دبر كل صلاة مكتوبة حلت له الشفاعة مني يوم القيامة اللهم أعط محمدا الوسيلة واجعله في المصطفين محبته، وفي العالين درجته وفي المقربين داره (المعجم الكبير للطبراني، الرقم: 7926، وفيه مطرح بن يزيد وهو ضعيف كما في مجمع الزوائد، الرقم: 16981، وقد تحرفت كلمة العالين إلى العالمين في المعجم الكبير ومجمع الزوائد كما نبه عليه الشيخ محمد عوامة في حاشيته على القول البديع صـ 363)
Abu Ummamah (radhiyallahu ‘anhu) anaripoti kwamba Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) kasema, “Mwenye kusoma maneno yafuatayo baada ya kila Swalah ya fardh, uombezi wangu utakuwa juu yake siku ya Qiyaamah:
اَللّٰهُمَّ أَعْطِ مُحَمَّدًا الْوَسِيْلَةَ وَاجْعَلْهُ فِيْ الْمُصْطَفَيْنَ مَحَبَّتَهُ وَفِيْ الْعَالِيْنَ دَرَجَتَهُ وَفِيْ الْمُقَرَّبِيْنَ دَارَهُ
Ewe Mwenyezi Mungu! Mfariji Muhammad (sallallahu ‘alaihi wasallam) waseelah (kuwa na haqqi ya uombezi siku ya Qiyaamah), na weka mapenzi yake katika (mioyo ya) waliochaguliwa, na umuweke kati ya walio juu kidaraja, na ufanye makazi yake miongoni mwa vipenzi vyako na walio karibu kwako.
Tukio la Mulla Jaami (rahimahullah)
Imepokelewa kwamba Mulla Jaami (rahimahullah) , pindi alikuwa ametunga qaseedah kwa mapenzi ya Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam), aliamua kuendelea na hajj.
Nia yake zaidi ilikuwa ni kusimama mbele ya Raudhah Mubaarak (kaburi la Nabii wa Allah (sallallahu ‘alaihi wasallam)) na asome shairi yake mbele ya Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) Baada ya kuhiji, alipokusudia kuondoka kwenda Madina Munawwarah, Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) alitokea katika ndoto kwa mkuu wa mkoa wa Makkah Mukarramah na kumwambia kwamba hatakiwi kumruhusu Mulla Jaami (rahimahullah) aingie Madinah Munawwarah. Mkuu wa mkoa wa Makkah Mukarrama akamkataza kuondoka kwenda Madina Munawwarah, hata hivyo mapenzi yake na hamu yake kwa Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) yalikuwa kwamba licha ya amri hiyo, alifunga safari kwa siri kuelekea Madinah Munawwarah.
Kwa mara nyingine tena, Mkuu wa mkoa wa Makkah Mukarrama aliona ndoto ambayo Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) alikuwa akimwambia kwamba Mulla Jaami (rahimahullah) ameondoka Makka, na asimruhusu kufika Madinah Munawwarah.
Wakati huu, Mkuu wa Makkah Mukarrama alituma watu wachache kumfuata ili wamrudishe. Walimkamata na kumtendea ukali zaidi kama wamemteka, na kisha wakamuweka gerezani.
Kwa mara ya tatu, Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) alitokea katika ndoto ya mkuu wa Makkah Mukarrama, akimkemea. Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) akamwambia kwamba Mulla Jaami (rahimahullah) hakuwa mhalifu (kwa hivyo, asitendewe ukali).
Hata hivyo, yote aliyoyafanya ni kwamba kutokana na mapenzi yake kwa Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam), alikuwa ametunga mashairi ambayo alikusudia kuyasoma mbele ya Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) akamwambia Mkuu wa Makkah Mukarrama kwamba kama angelisoma mashairi yake basi Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) angenyoosha mkono wake kupeana mkono wa Mulla Jaami (rahimahullah), na hii ingesababisha mkusanyiko mkubwa miongoni mwa watu.
Baada ya hayo, mkuu wa mkoa alimwacha huru na kumtendea heshima kubwa na kumfariji. (Fazaail-e-Durood Pg, 157)