عن جابر رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: من صلى علي مائة صلاة حين يصلي الصبح قبل أن يتكلم قضى الله تعالى له مائة حاجة يعجل له منها ثلاثين ويدخر له سبعين وفي المغرب مثل ذلك قالوا: وكيف الصلاة عليك يا رسول الله قال: إن الله وملائكته يصلون على النبي يأيها الذين آمنوا صلوا عليه وسلموا تسليما اللهم صل على محمد حتى تعد مائة (رواه أحمد بن موسى الحافظ بسند ضعيف كذا في القول البديع صـ ٣٦٤)
Sayyidina Jaabir (radhiyallahu ‘anhu) anasema kwamba Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) alisema:
“Mwenye kuniswalia mara mia moja mara tu baada ya kuswali Swalaah ya Alfajiri kabla ya kuongea basi Allah subhaana wata’ala atamtimizia mahitaji yake mia. Allah subhaana wata’ala Ataharakisha kutimia mahitaji thelathini (katika dunia hii), na Allah ataweka ukamilifu wa sabini katika Akhera, na hali kama hiyo itakuwa kama mtu atamswalia Nabii wa Allah (sallallahu ‘alaihi wasallam) baada ya Swalah ya Maghrib (yaani mtu atapokea fadhila zile zile). Maswahaba (radhiyallahu ‘anhum) wakauliza, “Tukuswalia vipi ewe Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) ?” Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) akasoma Aayah ifuatayo:
إِنَّ الله وَمَلئِٰكَتَهُ يُصَلُّوْنَ عَلٰى النِّبِيِّ يٰأَيُّهَا الَّذِيْنَ آمَنُوْا صَلُّوْا عَلَيْهِ وَسَلِّمُوْا تَسْلِيْمًا
Hakika Allah na malaika wake wanamswalia Nabii wa Allah (sallallahu ‘alaihi wasallam) Ewe mlioamini mswalieni Nabii wa Allah (sallallahu ‘alaihi wasallam) Kwa kumtumia salaam.
Baada ya hapo Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) akasema haya ifuatayo na akasema isomeni mara Mia moja:
اَللّٰهُمَّ صَلِّ عَلٰى مُحَمَّد
Kumswalia Nabii wa Allah (sallallahu ‘alaihi wasallam) kwenye Mkusanyiko
Mtunzaji wa Nuzhatul Majaalis anaeleza tukio ifuatayo kutoka kwa mchamungu fulani:
Nilikuwa na jirani ambaye alikuwa mwenye kufanya madhambi mengi. Nilikuwa nikimshauri kila wakati kutubu, lakini hakutaka kusikiliza. Baada ya kufariki nilimwona katika Jannah. Nilipomuuliza amefikaje Jannah alisema, “Wakati fulani nilikuwepo kwenye mkusanyiko wa Muhadith (Mwanachuoni wa hadith) aliyesema, ‘Mwenye Kumswalia Nabii wa Allah (sallallahu ‘alaihi wasallam) kwa sauti atahakikishiwa Jannah.’ Hivyo nikamswalia Nabii wa Allah (sallallahu ‘alaihi wasallam) kwa sauti, na wengine walifanya hivyo pia. Kwa hivyo sote tulisamehewa na Allah.” (Nuzhatul Majaalis 87/2)