عن ابن عباس قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: من قال جزى الله عنا محمدا صلى الله عليه وسلم بما هو أهله أتعب سبعين كاتبا ألف صباح (حلية الأولياء ٢/٣٠٦، وفي سنده هاني بن المتوكل وهو ضعيف كما في القول البديع صـ ١١٦)
Sayyidina ibn Abbaas (radhiyallahu ‘anhuma) anasimulia kwamba Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) alisema, “Yoyote atakayenitumia salaam ifuatayo, (akajishughulisha na) akawachosha malaika sabini (katika kurikodi thawabu ya salaam iliyosomwa) kwa siku elfu moja.”
جَزٰى اللهُ عَنَّا مُحَمَّدًا صَلّٰى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بِمَا هُوَ أَهْلُهُ
Allah subhaana wata’ala amlipe Nabii Muhammad (sallallahu ‘alaihi wasallam) kwa niaba yetu kama anavyostahili (yaani: thawabu inayostahili nafasi yake tukufu).
Baraka za Hadithi Mubaraka za Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam)
Shekhe Abu Ahmad, Abdullah bin bakr bin Muhammad (rahimahullah)، aliwahi kutaja, “maarifa ambayo yana baraka zaidi, ambayo ni maarifa makubwa zaidi, na yana faida zaidi katika ulimwengu huu na unaofuata, baada ya elimu ya kitaab cha Allah subhaana wata’ala, ni maarifa ya Hadithi Mubaraka ya Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) Mtu atapata baraka nyingi kupitia Hadithi Mubaraka kwa sababu ya salaam tele ambayo atasoma juu ya Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) wakati wa kusoma Hadithi Mubaraka. Hadithi Mubaraka za Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) ni kama bustani ambazo ndani yake utapata kila aina ya wema, haki, fadhila na dhikri.” (Al-Qawlul Badee, Pg,287)