Kupata Maombezi Ya Nabii Wa Allah (sallallahu ‘alaihi wasallam)

عن أبي الدرداء قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: من صلى علي حين يصبح عشرا وحين يمسي عشرا أدركته شفاعتي يوم القيامة (رواه الطبراني بإسنادين وإسناد أحدهما جيد ورجاله وثقوا كذا في مجمع الزوائد، الرقم: ١٧٠٢٢)

Sayyidina Abu Dardaa (radhiyallahu ‘anhu) ameripoti kwamba Nabii wa Allah (sallallahu ‘alaihi wasallam) amesema, “yoyote ambaye atakaye nitumie salaam mara kumi asubuhi na mara kumi jioni, atapata msaada wangu siku ya qiyama.”

Njia ya kupata maombezi ya Nabii Muhammad (sallallahu ‘alaihi wasallam)

Sayyidina Qutb Al halabi anasema:

Niliwahi kukutana na Abu ishaq, Abdullah bin ali bi atiyyah At-Taleedami (rahimahullah) akaniambia, “Nilibarikiwa na maono yaliyobarikiwa ya Nabiii Muhammad (sallallahu ‘alaihi wasallam) katika ndoto. Nilipomwona nikamuambia, ‘Ewe Nabii Muhammad (sallallahu ‘alaihi wasallam) nakuomba uniombee siku ya qiyamah’. Nabi muhammad (sallallahu ‘alaihi wasallam) alijibu, niswalie kwa wingi. (Al Qawlul Badee, Pg, 275)

About admin

Check Also

Chanzo cha nuru siku ya Qiyaama

عن ابن عمر رضي الله عنهما قال قال رسول الله صلى الله عليه وسلم زينوا …