Muharram na Aashura

Ni mfumo wa Allah ambao ametoa wema maalum na umuhimu kwa baadhi ya mambo juu ya mengine. kutoka kwa wanadamu, manabii wamebarikiwa na vyeo na hali ya juu ya wengine. kutoka sehemu tofauti ulimwenguni haramain shareefain (Makka mukarrama na madina munawwara) na musjid Alaqsa wamepewa daraja maalum juu ya ulimwengu wote. kutoka miezi kumi na mbili ya kalenda ya Kiisilamu, utakatifu maalum umepewa miezi minne yaani: Dhul qa’dah, Dhul hujjah muharram na Rajab. Hivyo hivyo kati ya siku za mwaka wa Kiislamu, siku ya Ashurah imebarikiwa na fadhila za kipekee na baraka kubwa.

Wakati mwezi wa dhul hijja umechaguliwa kwa ajili ya kutimiza tambiko la hajj na uchinjaji, mwezi wa muharram ni mwezi ambao umepata heshima ya kuwa mwezi wa Allah subhaana wata’alah na mwezi ambao una mfungo wa siku iliyobarikiwa ya Ashura. fadhila kubwa na nyingi baraka za siku hii zinaweza kueleweka kwa kiasi fulani kutoka kwa hamu ambayo Nabii Muhammad (sallallahu ‘alaihi wasallam) alionyesha kwa kusubiri kufika kwake.

عن ابن عباس رضي الله عنهما قال ما رأيت النبي صلى الله عليه وسلم يتحرى صيام يوم فضله على غيره إلا هذا اليوم يوم عاشوراء

Abdullah bin Abbas anaripoti: “Sikumuona Nabii Muhammad ﷺ anasubiri kwa hamu kufunga kwa siku yoyote nzuri kuliko siku ya ashurah” (Saheeh Bukhaari #2006)

عن أبي قتادة رضي الله عنه قال قال رسول الله صلى الله عليه وسلم صيام يوم عاشوراء إني أحتسب على الله أن يكفر السنة التي قبله

imeripotiwa kutoka kwa Abu qatadah (radhiyallahu ‘anhu) kwamba Nabii Muhammad (sallallahu ‘alaihi wasallam) alisema ‘kwa sababu ya kuzingatia mfungo wa siku ya Ashura, nina matumaini kwamba Allah subhaana wata’alah atafutiliya mbali dhambi za mwaka uliopita’. (Ibnu Maajah #1738, Saheeh Muslim #1162)

Malipo ya kufunga mwezi mzima

Mwezi wa muharram unachukuliwa kama mwezi wa Allah subhaana wata’alah na mfungo unaozingatiwa ndani yake unahesabiwa kama mfungo bora baada ya mwezi wa Ramadhaan. Ni fadhila ya kipekee ya mwezi wa muharram kwamba kwa kila mfungo ambao mtu kufunga, mtu hupokea thawabu ya kufunga mwezi mzima. hii thawabu ni ya kipekee kwa mwezi wa muharram kwa sababu hakuna mwezi mwingine unaopata fadhila hii.

عن ابن عباس رضي الله عنهما قال قال رسول الله صلى الله عليه و سلم : من صام يوم عرفة كان له كفارة سنتين ومن صام يوما من المحرم فله بكل يوم ثلاثون يوما

Imeripotiwa kutoka kwa Abdullah bin Abbas-(radhiyallahu ‘anhuma) kwamba Nabii Muhammad (sallallahu ‘alaihi wasallam) alisema ‘yule atakae funga mfungo wa siku ya arafah atasamehewa miaka miwili ya dhambi zake, na yule anayefunga katika mwezi wa muharram, kwa kila siku atakayofunga atapata thawabu ya kufunga mwezi mzima. (At-Targheeb wat-Tarheeb #1529)

عن أبي هريرة رضي الله عنه قال قال رسول الله صلى الله عليه وسلم أفضل الصيام بعد رمضان شهر الله المحرم وأفضل الصلاة بعد الفريضة صلاة الليل

inaripotiwa kutoka kwa Abu hurairah (radhiyallahu ‘anhu) kwamba Nabii Muhammad (sallallahu ‘alaihi wasallam) alisema ‘mfungo bora wa kufunga baada ya mwezi wa Ramadhaan, ni mfungo wa mwezi wa Allah subhaana wata’alah mwezi wa muharram, na sala bora baada ya faraaidh (salaah ya lazima) ni sala ya tahajjud. (Saheeh Muslim #1163)

Mfungo Wa Sunna Wa Aashura

Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) alifunga siku ya aashura na akawahimiza maswahaaba (radhiyallahu ‘anhum) pia kufunga. Kiwango cha shauku na jazba ambayo maswahaba (radhiyallahu ‘anhum) walishikilia sunna hii ya Mubarak labda inaweza kupimwa kutoka Hadiyth ifuatayo.

عن الربيع بنت معوذ بن عفراء رضي الله عنها قالت فكنا بعد ذلك نصومه ونصوم صبياننا الصغار منهم إن شاء الله ونذهب إلى المسجد فنجعل لهم اللعبة من العهن فإذا بكى أحدهم على الطعام أعطيناهم إياه عند الإفطار

Rubayyi (radhiyallahu ‘anhu) anaripoti kuwa maswahaba (radhiyallahu ‘anhum) walifunga siku ya aashura na pia waliwahimiza watoto wao kuizingatia. Maswahaba (radhiyallahu ‘anhum) walikuwa wakiwatengenezea watoto wao vitu vya kuchezea na ikiwa mtoto yoyote anahisi njaa na kulilia chakula, walikuwa wanawapa vitu vya kuchezea ili wajishughulishe mpaka wakati wa kufuturu.(Saheeh Muslim #1136)

Historia ya Aashura

Kabla ya hijrah, Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) alikuwa akifunga fungo la aashura huko Makkah Mukarrama. baada ya kuhamia Madina Munawwarah, Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) alishuhudia mayahudi wakifunga siku ya aashura. Wakati Nabii Muhammad (sallallahu ‘alaihi wasallam) alipouliza kutoka kwao sababu ya wao kufunga, walielezea kuwa ilikuwa juu ya hii Siku ambayo Allah subhaana wata’alah alimwokowa Moosa (alahimus salaam) na Bani Israeel kutoka kwa jeuri na ukandamizaji wa Firoun na watu wake na Allah subhaana wata’ala akawaadhibu firoun na jeshi lake.

عن ابن عباس رضي الله عنهما قال قدم النبي صلى الله عليه وسلم المدينة فرأى اليهود تصوم يوم عاشوراء فقال ما هذا قالوا هذا يوم صالح هذا يوم نجى الله بني إسرائيل من عدوهم فصامه موسى قال فأنا أحق بموسى منكم فصامه وأمر بصيامه

Abdullah bin abbaas (radhiyallahu ‘anhuma) ameripoti: “wakati Nabii Muhammad (sallallahu ‘alaihi wasallam) alipohamia madina munawwarah, alishuhudia mayahudi wakifunga fungo la aashura. Baada ya kuuliza, walijibu kwamba hii ilikuwa siku nzuri na hii ndiyo siku ambayo Allah subhaana wata’ala alikuwa amewakabidhi bani israeli kwa usalama kutoka kwa adui dhaalimu (firoun na jeshi lake). Kwa kumuonesha shukrani Allah subhaana wata’ala, Moosa (alahimus salaam) alifunga siku hii. Nabii Muhammad (sallallahu ‘alaihi wasallam) alisema, “tunastahili kumfuata Moosa (alahimus salaam) kuliko nyie”. baadaye, Nabii Muhammad (sallallahu ‘alaihi wasallam) aliendelea kufunga siku hii na akawaamrisha maswahaba pia wafunge.”(Saheeh Bukhaari #2004)

kabla ya mfungo wa Ramadhaan kuwa wa lazima, kufunga siku ya aashura ilikuwa fardh (lazima). Baada ya mfungo wa Ramadhaan kuwa wa lazima, kufunga siku ya aashura ilitangazwa kuwa hiari (sunnah).

عن عائشة زوج النبي صلى الله عليه وسلم أنها قالت :كان يوم عاشوراء يوما تصومه قريش في الجاهلية وكان رسول الله صلى الله عليه و سلم يصومه في الجاهلية فلما قدم رسول الله صلى الله عليه وسلم المدينة صامه وأمر بصيامه فلما فرض رمضان كان هو الفريضة وترك يوم عاشوراء فمن شاء صامه ومن شاء تركه

Aaisha (radhiyallahu ‘anha) alikuwa ameripoti: “katika zama za kabla ya uisilamu, maquraish walikuwa wakifunga siku ya aashura. Nabii Muhammad (sallallahu ‘alaihi wasallam) pia alifunga mfungo wa aashura. Baada ya kuhamia madina munawwarah, Nabii Muhammad (sallallahu ‘alaihi wasallam) aliendelea na mazoezi haya mazuri (ya kufunga siku ya aashura) na kuwaamrisha maswahaba kufunga hii siku nzuri (kwa sababu ulikuwa mfungo wa lazima). Lakini, baada ya mfungo wa Ramadhaan kuwa fardh, kufunga siku ya aashura haukubaki tena fardh. “(badala yake ilifanywa kuwa sunna (hiari)).(Muatta Imaam Maalik #842)

kuweka funga ya aashura kwa hivyo ilibaki kuwa mazoea ya rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) na maswahaba (radhiyallahu ‘anhum) hadi mwisho wa maisha ya rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) Lakini, kabla ya kufariki kwake, rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) aliwaamuru maswahaba wawapinge mayahudi kwa kuongeza siku nyingine ya kufunga kwa mfungo wa aashura.

عن ابن عباس رضي الله عنه قال قال رسول الله صلى الله عليه وسلم صوموا يوم عاشوراء وخالفوا فيه اليهود صوموا قبله يوما أو بعده يوما

Abdullah bin abbaas (radhiyallahu ‘anhuma) anaripoti kuwa rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) alisema: “fungeni mfungo wa aashura na uwapinge mayahudi kwa kufunga pia siku moja kabla au baada yaani: siku ya tisa na ya kumi au siku ya kumi na ya kumi na moja ya muharram (As-Sunanul Kubra lil Baihaqi #8406, At-Talkheesul Habeer #931)

Somo la Aashura

Pamoja na mfungo wa Aashura kuwa njia ya kuvuna fadhila kubwa, pia inasisitiza na kufundisha somo muhimu. Hili ni somo la kudumisha utambulisho wa Kiislam wakati wote na kujiepusha kabisa na kuwaiga makuffaar (makafiri, mayahudi na Wakristo) katika tamaduni zao. Kwa hivyo, Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) aliagiza ummah kufunga kwa siku mbili (yaani: siku ya tisa na ya kumi au siku ya kumi na ya kumi na moja) ili kuwapinga mayahudi.

Wakati inaonekana kama tumewaiga mayahudi katika kufunga (ambayo ilikuwa ibaada) haikupendwa sana na Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam), mtu anaweza kufikiria ni kiasi gani zaidi Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) hakupenda ummah wake kuiga makafiri katika tamaduni zao, mavazi, mambo ya maisha yao na mengineyo. Kuiga “njia za makuffaar” ambayo inajulikana kama ‘tashabbuh’, ni marufuku kabisa katika Uislamu kwani inadhihirisha kwamba mtu anajihusisha na njia na utamaduni wa maadui wa Uislamu na kupinga njia ya Mubarak ya Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) kuwaiga makuffaar kumetengwa sana ndani ya Uislamu na Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) ametangaza:

عن ابن عمر قال قال رسول الله صلى الله عليه وسلم من تشبه بقوم فهو منهم

“Yule anayeiga watu atahesabiwa kati yao.”(Abu Dawood #4033)

Hakuna mtu anayechagua kufanana na yule ambaye ni adui yake. Badala yake, wote wanapendelea kufanana na wale wanaowapenda. Mfuasi wa kweli wa Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) kwa hivyo atapenda kufanana na kuiga mpendwa wake. Atapenda kujitambulisha na Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam), sio na wale ambao ni maadui wa Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) na Waislamu.

Mavazi

Kuwaiga makuffaar kunaweza kutokea katika nyanja nyingi za maisha. Lakini, dhahiri zaidi ipo katika hali ya kuonekana na mavazi. Mwonekano wa uvaaji ambao mtu anapitisha hufanya iwe dhahiri ni nani anamtambulisha. Zaidi ya hayo, inashuhudiwa kwa ujumla kuwa mavazi ambayo mtu huvaa huathiri tabia na mwenendo wa mtu. Hivyo hivyo, kanuni na maadili ya mtu hutengenezwa pole pole na kulingana na mavazi yake. Ushawishi wa kuonekana na mavazi ni muhimu sana hata makuffaar hugundua athari zake. Kupigwa marufuku kwa wanawake wa Kiislam kuvaa mitandio na hijaab katika nchi zingine ni ushahidi wazi wa hii na inazungumzia ukweli kwamba mavazi na sura ya Kiislamu ina athari kubwa kwa wengine. Makuffaar kwa hivyo wanataka kupiga marufuku utambulisho unao onekana wa uislamu na kuwalazimisha kufuata njia na tamaduni zao. Allah subhaana wata’ala anasema:

وَلَن تَرضىٰ عَنكَ اليَهودُ وَلَا النَّصـٰرىٰ حَتّىٰ تَتَّبِعَ مِلَّتَهُم

Mayahudi na Wakristo hawataridhika nawe isipokuwa ufuate dini yao.(Surah Baqarah, Aayah 120)

Kwa hivyo wakati uvaaji na muonekano uliofundishwa na Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) hauzingatiwi na makuffaar kuigwa, mara nyingi inakuwa ngumu au hata haiwezekani kutofautisha Mwislamu kutoka kwa Mayahudi, Mkristo au Mtu asiyemuamini Mungu.

Mazoea yasiyo na msingi

Kuna mila na desturi nyingi ambazo hazina msingi ambazo watu hushiriki katika tarehe kumi ya Muharram. Miongoni mwa mila na mazoea haya yasiyo na msingi ni kuomboleza juu ya kuwawa kwa Hussain-(radhiyallahu ‘anhu) kuwawa kwa Hussain (radhiyallahu ‘anhu) bila shaka ilikuwa miongoni mwa matukio mabaya na ya kuvunja moyo yaliyotokea katika historia ya uislaam. Lakini licha ya hayo, inapaswa kueleweka kuwa hafla ya Aashura na fadhila zake hazihusiani na kuwawa shahidi kwa Hussain (radhiyallahu ‘anhu) badala yake, Aashura ulikuwa umepokea fadhila na uzuri wake hata kabla ya kuzaliwa kwa Hussain (radhiyallahu ‘anhu) Kwa hivyo desturi ya kuomboleza kuwawa kwa Hussain (radhiyallahu ‘anhu) na mashia haina msingi yoyote katika Uislamu .

Fadhila ya matumizi kwa familia ya mtu siku ya aashura

Mbali na fadhila ya siku ya Aashura, Nabi Muhammad (sallallahu ‘alaihi wasallam) pia amehimiza kwamba mtu anapaswa kuwa mkarimu zaidi kwa familia yake katika siku hii nzuri na ajitolee juu yao.

عن أبي هريرة رضي الله عنه أن رسول الله صلى الله عليه و سلم قال من أوسع على عياله وأهله يوم عاشوراء أوسع الله عليه سائر سنته (قال المنذرى في الترغيب: رواه البيهقى و غيره من طرق وعن جماعة من الصحابة وقال البيهقي:هذه الأسانيد وإن كانت ضعيفة فهي إذا ضم بعضها الى بعض أخذت قوة والله أعلم)

Abu Hurairah (radhiyallahu ‘anhu) anaripoti kwamba Nabii Muhammad (sallallahu ‘alaihi wasallam) anasema, “Yoyote anayetoa kwa hiari juu ya familia yake siku ya Aashura, Allah subhaana wata’ala atambariki kwa riziki nyingi kwa mwaka mzima.”(At-Targheeb wat-Tarheeb #1536)

About admin

Check Also

Sunna Na Adabu Za Dua 8

19. Jiepushe na ulaji wa haramu au chakula chenye mashaka na kujihusisha na madhambi. Mtu …